MAAFA YA USHURU

Mteja anunua sukari iliyochanganywa na Unga kwenye duka, Tharaka Nithi

“Nitatoa wapi faida mimi? Hii ni Kenya na tunaishi kulingana na hali” - mwenye duka alisema.

Muhtasari

• Kulingana na mkewe Jonah, robo kilo ya sukari inatosha kwa vikombe nane vya chai, ila siku hiyo ilikuwa tofauti, maana aliandaa vikombe sita na sukari hiyo haikutosha.

Sukari
Sukari
Image: star

Huku malalamiko ya kupanda kwa gharama ya maisha yakiendelea kusikika kila uchao, kaunti ya Tharaka-Nithi maajabu yameshuhudiwa ambapo mteja anayejulikana kwa jina Jonah alielekea katika duka moja na kuagiza sukari robo kilo ya kuandalia jamaa zake chai.

Kwa kawaida, alikuwa mteja wa kila siku maana duka hilo linaaminiwa kuwajali wateja kwa kuuza bidhaa kwa bei nafuu na kwa kila kiwango. 

Juni 28, Jonah alifika nyumbani huku sukari yake aliyonunua kwa shilingi 35 ameibeba mkononi bila bila kupoteza wakati wowote mkewe akaanza mandalizi ya chai asubuhi, kabla ya kuondoka kusaka riziki ya siku.

Kulingana na mkewe Jonah, robo kilo ya sukari inatosha kwa vikombe nane vya chai, ila siku hiyo ilikuwa tofauti, maana aliandaa vikombe sita na sukari hiyo haikutosha.

“Leo nilipika chai vikombe sita, na kawaida mimi hupika vikombe nane. Nilishangaa sukari haitoshi, ilikuwa nyingi sana na haikutosha kwa chai yetu. Sikujali maana hata baada ya kutumia sukari yote ilibakia duvia. Nilijionea maajabu nilipokuwa naichunga, unga ndio ulisalia ndani ya kichungi na sufuria, nikashangaa unga umetoka wapi.”  Alisimulia bibiye Jonah.

Bila ya kuupoteza muda wowote, mumewe alienda moja kwa moja hadi kwa hilo duka alipomkuta muuzaji bado anawahudumia wateja wengine.

Sukari ya leo kwani imeongezwa nini mkuu? ” Aliuliza Jonah, ambaye mfukoni kulikuwa na karatasi iliyobeba chembechembe za unga ambazo mkewe alizichuja kwenye chai.

Akimjibu mteja, mwuuzaji alieleza kuwa hali ya uchumi nchini imedorora, pia sukari yenyewe nchini haipatikani. Alimweleza waziwazi kuwa ilikuwa kwa hiari kuchanganya sukari yangu na unga ili tuweze kuishi. “ Nitatoa wapi faida? pia nami nina watoto wa CBC ninaowaelimisha. Lazima pia nilipe ushuru, hii ni Kenya na ni lazima tuishi kulingana na hali.” Alieleza Elvis mwuuza duka.