HALI YA UCHUMI

Hakuna ahadi hata moja ya Kenya Kwanza imetimia - Eric Omondi adai

"Binafsi kama Eric Omondi, naipatia mwezi mmoja unusu, hali ikiendelea namna ilivyo Wakenya wataamka!," Eric alisema.

Muhtasari

•Mkuza maudhui huyo alikiri kwamba tayari uchungu umeshuhudiwa kwa Wakenya, kutokana na kupandishwa kwa nauli kwa wahudumu wa matatu, akidakia jinsi serikali tawala analazimisha sera zake kwa Wakenya.

DOUGLAS OKIDY
Image: Mchekeshaji Eric Omondi

Mkuza maudhui Eric Omondi amedai kwamba serikali inayotawala ya Kenya Kwanza chini ya Rais Ruto iliwahadaa wananchi wakati wa kampeni.

Msanii huyo ameeleza kuwa Kenya Kwanza ilitumia kauli za mama mboga na mtu wa bodaboda ili kujizolea kura lakini sasa mambo si kama jinsi walivyosema .

Katika mahojiano na runinga ya KTN, Eric Omondi alisema kuwa serikali tawala ilisema kuwa itawakilisha watu maskini iliyowarejelea kuwa mama mboga na mtu wa bodaboda, ila, na kufikia zaidi ya miezi kumi sasa hakuna hata moja kati ya ahadi zake imetekeleza, kinachokusudiwa, ni gharama ya juu ya maisha inayochangiwa na kupanda kwa bei ya bidhaa.

Binafsi huu ndio mpango wangu kama Eric Omondi, unajua, petroli ikipanda kila kitu kitapanda bila shaka, wabunge pia wamewataliki Wakenya waliowachagua, wanaitumikia serikali, serikali yenyewe imekiri kuwa itawahudumia waliopigia kura mswada wa fedha 2023 wakikubaliana na mswada huo,” alieleza KTN.

Mkuza maudhui huyo alikiri kwamba tayari uchungu umeshuhudiwa kwa Wakenya, kutokana na kupandishwa kwa nauli kwa wahudumu wa matatu, akidakia jinsi serikali tawala analazimisha sera zake kwa Wakenya.

Msanii huyo ambaye alieleza kufurahishwa na uamuzi wa mahaka kuhusu uteuzi wa CAS’s, alikiri kwamba inawezekana kuwahamasisha raia kuungana ili waweze kutetea haki zao.“ Tukimaliza mwaka mmoja, tutawahamasisha raia, tuelekee moja kwa moja hadi ikulu iwapo hali ilivyo kwa sasa haibadilika katika kipindi cha mwezi mmoja ujao. Inaweza kuonekana ucheshi kwa maana mimi ni mcheshi lakini saa hii, nakiri kwa uyakini,”aliendelea.

Eric Omondi alieleza hayo alipotoka Dodoma, Tanzania, alikoenda kuomba pesa za msaada ili kuweza kuwasaidia Wakenya wanaoangamia humu nchini kutokana na bei ghali ya bidhaa inayoendelea kushuhudiwa.