Spotify yaingia vitani na YouTube na TiKTok kuhusu hatua ya kupakia video

Spotify wanalenga kuzindua uwezo wa mtumiaji kupakia video ndefu kwenye jukwaa hilo kama njia moja ya kukimu mahitaji makubwa ya video kwa kizazi cha Gen Z.

Muhtasari

• Kwa kugundua mapungufu yao katika kuruhusu watumiaji kuweza kuona video, Spotify inatajwa kuwahusisha washikadau mbalimbali kufanikisha hili.

Spotify vitani dhidi ya TikTok na YouTube.
Spotify vitani dhidi ya TikTok na YouTube.
Image: Facebook

Jukwaa la kupakia kazi za muziki la Spotify lina mpango wa kuzindua upakiaji wa video nzima kwenye kabrasha lake la video – hatua ambayo imetajwa kuwa itazua vita vikali baina ya Spotify na mitandao mingine kama TikTok na YouTube, jarida la Bloomberg limeripoti.

Spotify, jukwaa maalum ya utiririshaji wa miziki, wanaripotiwa kutathmini jinsi watakavyoanzisha upakiaji wa video nzima, hatua ambayo itazua ushindani mkali baina yao na jukwaa la YouTube ambalo kwa muda mrefu limekuwa likijulikana kwa upakiaji wa video ndefu, lakini pia TikTok ambao hivi karibuni walizindua kipengele cha kumkubalia mtumiaji kupakia video ya dakika hadi 5.

Kwa kunukuu taarifa amabzo ziko karibu na suala hilo, jarida la Bloomberg limeangazia jinsi ambavyo hatua hiyo itaipaisha Spotify katika ushindani mkali kwenye soko la miziki duniani.

Kufikia sasa, Spotify huwaruhusu watumiaji tu kupakia picha pekee kama utambulisho wa sura kwa kazi zao ambazo huwa ni za sauti pekee.

Kwa kugundua mapungufu yao katika kuruhusu watumiaji kuweza kuona video, Spotify inatajwa kuwahusisha washikadau mbalimbali kufanikisha hilo, hatua ambayo itawafaidi pakubwa kizazi cha Gen Z ambao wanapenda sana kufuatilia Sanaa ambayo ina picha na video ili kuhakiki na kushuhudia matukio wenyewe – kama ambavyo wanafanya TikTok na YouTube.

Hata hivyo, Bloomberg haikuweza kubaini ni lini haswa hatua hiyo itafanikishwa kwenye jukwaa lao.