Dereva aliyembeba Raila avunja kimya, alalamika wanafamilia wanamsumbua wakidai 'zawadi' alizotunukiwa

Murage alifichua kuwa kiongozi huyo wa ODM alilipa nauli ya basi kama wasafiri wengine wa kawaida.

Muhtasari

•Murage alisema kuwa ilikuwa mshangao mkubwa kuona mmoja wa wanasiasa wakuu wa Kenya akiabiri basi lak

•Murage anasema akipewa kazi ya kumuendesha mwanasiasa huyo tajika ataichukua na kuifanya kwa bidii.

amevunja kimya kuhusu kumbeba Raila Odinga katika mahojiano na KTN News.
Duncan Murage amevunja kimya kuhusu kumbeba Raila Odinga katika mahojiano na KTN News.
Image: HISANI

Duncan Murage, dereva wa basi lililombeba mwanasiasa Raila Odinga hadi jijini Nairobi siku ya Jumatatu amesema kiongozi huyo wa chama cha ODM alipanda gari lake kama abiria wa kawaida tu.

Katika mahojiano na KTN News, dereva huyo wa matatu alisema kuwa alikuwa katika shughuli zake za kila siku za kuwasafirisha abiria kutoka mji wa Ngong hadi Nairobi CBD na kurudi wakati kiongozi huyo wa Azimio la Umoja-One Kenya aliposimamisha basina kupanda.

“Alisimamisha gari, sisi tulimshtukia tu, akaingia tu kama mtu wa kawaida tukambeba. Vile tu sisi huwa tunakuja tukabeba watu, tukaenda hadi GPO akashuka,” Murage alisimulia.

Alisema baada ya kiongozi huyo wa ODM kuingia ndani ya basi hilo kulikuwa na msisimko na kelele nyingi huku watu wenye shauku wakikusanyika kujua kinachoendelea.

Murage ameeleza kuwa yeye hata hivyo aliendelea kuendesha basi hadi jijiini jinsi tu huwa anafanya katika siku za kawaida huku Raila akitangamana na wasafiri wengine upande wa nyuma.

“Ata sikupata nafasi ya kuongea na yeye. Aliingia tu huko nyuma kama mtu wa kawaida. Sikuogopa juu mimi ni mtu wa kawaida tu. Vile sisi hubeba watu tu, niliendesha gari tu hivyo,” alisema.

Murage alisema kuwa ilikuwa mshangao mkubwa kuona mmoja wa wanasiasa wakuu wa Kenya akiabiri basi lake hadi mjini na akakiri kwamba ilimletea msisimko mkubwa moyoni mwake.

Pia alifichua kuwa mgombea huyo wa urais katika uchaguzi uliopita alilipa nauli ya basi kama wasafiri wengine wa kawaida.

“Kila mtu alijisort kwa gari. Alijilipia,” Murage alisema.

Licha ya kulijengea jina basi lake kwa kuliabiri kwenda kazini, Murage analalamika kuwa baadhi ya watu wake wa karibu wamekuwa wakimsumbua kwa simu wakijaribu kunufaika na pesa ambazo wanafikiri kiongozi huyo wa ODM aliwazawadia siku ya Jumatatu.

“Wanasema Baba alitujenga lakini hakuna kitu kama hicho. Alibebwa tu kama mtu wa kawaida. Gari imepata tu hype,” alisema.

Murage anasema akipewa kazi ya kumuendesha mwanasiasa huyo tajika ataichukua na kuifanya kwa bidii.