MAANDAMANO YA AZIMIO

Azimio waapa kuendeleza maandamano yao wiki ijayo siku tatu

Tutaandamana wiki ijayo Jumatatu, Jumanne na Jumatano hadi Kenya Kwanza isikie Wakenya - Sifuna

Muhtasari

•Maandamano ya Jumatano yaliacha mali chungu nzima huku watu 9 wakiripotiwa kupigwa risasi na kuiaga dunia.

Kinara wa upinzani akiandamana na raia katikakati mwa jiji la Nairobi, Julai 10
Kinara wa upinzani akiandamana na raia katikakati mwa jiji la Nairobi, Julai 10
Image: Raila Odinga// TWITTER

Viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya wameapa kuendeleza maandamano hadi pale serikali tawala ya Kenya Kwanza itakaposikia matakwa ya Wakenya kuangazia hali ngumu inayowakumba ya maisha.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha runinga ya Citizen mapema Alhamisi 13, seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna alikiri kwamba serikali ya Kenya Kwanza haiwezi ikatoa amri ya kukamatwa kwa kiongozi wao Raila Odinga.

Sifuna alisema kuwa kuanzia wiki ijayo wataandaa maandamano siku tatu zikifuatana kutoka Jumatatu hadi Jumatano mpaka rais Ruto awasikize Wakenya.

Kenya Kwanza haiwezi ikatoa amri ya kukamatwa kwa Raila Odinga. Kuanzia wiki ijayo, tutakuwa na siku tatu za kufanya maandamano kutoka Jumatatu hadi Jumatano hadi wakati Rais Ruto awasikize Wakenya,” Alisema Sifuna kwenye mahojiano hayo.

Haya yanajiri wakati ambapo maandamano ya Jumatano 12 alisababisha hasara tele, zikiwemo kuaribiwa kwa mali yasiyokadirika na watu kuiaga dunia kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Licha ya hayo maandamano ya wiki jana Ijumaa ya Saba Saba pia yaliacha watu zaidi ya watano wakiwa wamefariki huku idadi isiyojulikana ikiachwa na majeraha katika makabiliano kati ya raia na maafisa wa usalama.

Hata hivyo, mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala amekiri kuwa kinara wa Azimio pia naye anafaidika na serikali hiyohiyo anayoivuruga, huku akieleza kuwa angepunguza mahitaji yake ili asaidie serikali kutatua suala la uchumi.

Raila Odinga ananufaika na serikali hii tu anayovuruga kila siku. Anayo magari sita ambayo yanagharamiwa na serikali, kama ni muungwana wacha apunguze yawe matatu ili asaidie serikali kutatua suala la uchumi,”  Malala aliposti katika mtandao wake wa Twitter.

Muungano wa Azimio bado ungali unaendelea na zoezi lao la kukusanya saini ambazo zitasaidia kuibandua serikali ya Rais Ruto mamalaki, huku muungano huo ukilenga kukusanya zaidi ya saini milioni 10.