Umetuchosha pia- Ichungw'a ampasha Raila kuhusu maandamano ya siku 3

Kulingana na Ichung'wah, Wakenya wamechoka na Raila anafaa kuwa tayari kwa kile kitakachokuja.

Muhtasari
  • Upinzani umewataka Wakenya kutoka matabaka mbalimbali kujitokeza kwa wingi na kutoa kauli dhidi ya serikali ya Rais William Ruto.
  • Matamshi ya Ichung'wah kwenye Twitter yalikuwa kujibu uthibitisho wa Raila kwamba maandamano bado yataendelea.
KIMANI ICHUNGW'A
Image: TWITTER

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung'wah amemkashifu kiongozi wa Azimio Raila Odinga kuhusu maandamano yaliyopangwa ya siku tatu kuanzia Jumatano.

Kulingana na Ichung'wah, Wakenya wamechoka na Raila anafaa kuwa tayari kwa kile kitakachokuja.

Mbunge huyo wa Kikuyu alisisitiza kwamba usaliti hautampeleka Waziri Mkuu huyo wa zamani popote pale na kwamba hakutakuwa tena na wizi na uharibifu wa mali.

Matamshi ya Ichung'wah kwenye Twitter yalikuwa kujibu uthibitisho wa Raila kwamba maandamano bado yataendelea.

Kiongozi huyo wa Upinzani katika ukurasa wake wa twitter Jumatatu jioni alisema Wakenya wanapaswa kujiandaa kwa maandamano ya kubadilisha mchezo.

"Kuanzia Jumatano, uwe tayari kwa Maandamano ya kubadilisha mchezo," Raila alisema.

Upinzani umewataka Wakenya kutoka matabaka mbalimbali kujitokeza kwa wingi na kutoa kauli dhidi ya serikali ya Rais William Ruto.

Upinzani unapinga gharama ya juu ya maisha na ushuru wa juu na utawala wa Kenya Kwanza, ulioletwa na Sheria ya Fedha, 2023.

Mahakama ya Juu ilisitisha utekelezaji wa Sheria hiyo, ambayo ilikuwa ya kwanza chini ya Rais William Ruto.

Viongozi wa matabaka mbalimbali wamekuwa wakimtaka Raila kusitisha maandamano yaliyopangwa na kutoa fursa ya mazungumzo.