MP Babu Owino amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa DCI

Owino amekamatwa muda mchache baada ya viongozi wakuu wa Azimio kudai kuwepo njama ya kuuawa na serikali baada ya kupokonywa ulinzi wao.

Muhtasari

• Kukamatwa kwake kunakuja saa chache baada ya viongozi wakuu katika mrengo wa Azimio kudai kuwepo kwa njama ya ya kuuawa.

babu Owino adai kukamatwa.
babu Owino adai kukamatwa.
Image: FACEBOOK

Mbunge Babu Owino wa Embakasi Mashariki amedia kukamatwa na makachero wa DCI tawi la uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA alipokuwa safarini kurejea Nairobi kutoka Mombasa.

Owino  kupitia ukurasa wake wa Facebook alidai kwamba makachero hao walimzuilia na kumweka chini ya ulinzi na mpaka alipokuwa anachapisha ujumbe huo, hakuwa ameambiwa makosa yake ni yepi.

“Nimezuiliwa na DCI JKIA baada ya kuwasili kutoka Mombasa. Kwa sasa nimefungwa,” Babu Owino alisema.

Kukamatwa kwake kunakuja saa chache baada ya viongozi wakuu katika mrengo wa Azimio kudai kuwepo kwa njama ya ya kuuawa kwao baada ya serikali kuondoa ulinzi wao.

Viongozi hao wakiongozwa na Martha Karua na Kalonzo Musyoka Jumanne katika mkutano wa vyombo vya habari walisema kwamba serikali imeondoa ulizni wao, hatua waliyoitaja kinyume na katiba kwa serikali kutoa ulinzi kwa kiongozi yeyote aliyewahi kuhudumu katika ngazi za juu za serikali kama waziri mkuu, Raila Odinga na makamu wa rais Kalonzo Musyoka kwa wakati mmoja kabla ya kuasisiwa kwa katiba moya ya 2010.

Kukamatwa kwa Owino ambaye ni mmoja wa wakereketwa wa sera za Upinzani kunakuja wakati ambapo wafuasi wa mrengo huo wanajiandaa kujitokeza barabarani kote nchini kuandamana katika kile ambacho Azimio wamesema kuwa ni uongozi dhalimu wa rasi Ruto lakini pia kupanda kwa gharama ya maisha humu nchini.

Odinga mapema aliwataka wafuasi wake kutoyumbishwa na taarifa za uongo kwamba maandamano yamesitishwa, akisema kuwa maandamano yao yataendelea kama yalivyoratibiwa na yanatarajiwa kuendelea kwa siku tatu mfululizo ili kumshinikiza Ruto kuridhia na matakwa yao.

Usiku wa Jumanne, serikali ilitangaza kufungwa kwa shule za kutwa za msingi na upili katika kaunti za Mombasa na Nairobi ili kuwalinda wanafunzi kutokana na athari zozote zinazoweza kutokea wakati wa makabiliano baina ya polisi na waandamanaji, kwani Ruto wikendi iliyopita alisimama tisti na kusema kuwa hakutakuwa na maandamano akiyataja kuwa kinyume cha sheria.