Maeneo Azimio ilifanya mkesha wa kuwasha mishumaa kuwakumbuka wahanga wa maandamano

Azimio mapema wiki hii walipiga breki maandamano yaliyoratibiwa Jumatano ili kutoa nafasi kwa wafuasi wao kuwasha mishumaa sehemu mbalimbali kuwakumbuka waliongamania katika vurugu.

Muhtasari

• Katika kaunti ya Mombasa, wafuasi wa Azimio walikongamana katika eneo la Pembe za Ndovu lakini awali walivurugana na polisi waliojaribu kuwatawanya.

• Nairobi hafla hiyo ilifanyika katika maeneo mbali mbali ikiwemo Mathare, Jacaranda, Kawangware na wakfu wa Jaramogi.

Mkesha wa kuwasha mishumaa.
GRAFIKI: Mkesha wa kuwasha mishumaa.
Image: HILLARY BETT