Moses Kuria awasifia Ruto na Raila kwa kukutana

Alibainisha kuwa serikali yake iko tayari kushirikisha upinzani mradi tu gharama ya maisha ibaki nje ya mjadala.

Muhtasari
  • Waziri huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliwataja wawili hao kama wakubwa wake kwa kubuni mwafaka wa kusitisha maandamano kote nchini.
CS Kuria atoa kauli ya ukakasi kuhusu maandamano ya Jumatano.
MAANDAMANO CS Kuria atoa kauli ya ukakasi kuhusu maandamano ya Jumatano.
Image: Twitter

Waziri wa Biashara Moses Kuria amelegeza msimamo wake dhidi ya shughuli za aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga baada ya kukubali mazungumzo na Rais William Ruto.

Waziri huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter aliwataja wawili hao kama wakubwa wake kwa kubuni mwafaka wa kusitisha maandamano kote nchini.

Alibainisha kuwa iwapo mazungumzo hayo yatafanyika, sekta ya uwekezaji nchi nzima itapata manufaa.

Mbunge huyo wa zamani wa Gatundu Kusini, hata hivyo, alisisitiza kuwa bado anapinga handshake na hatakubali ombi la upinzani la kutaka serikali iundwe.

"Kurejeshwa kwa mazungumzo ya pande mbili ni habari njema kwa Uwekezaji na uchumi kwa ujumla. Vurugu sio njia ya kutatua tofauti za kisiasa.

"Ni wakati wa kuunganisha pamoja kama taifa lenye serikali dhabiti na hata upinzani mkali ili kutuzuia. Kwa wakuu wangu William Ruto na Raila Odinga mko upande sahihi wa historia," alisema.

Kauli ya Kuria ilithibitisha yale ya Mkuu wa Nchi ambaye, alipokuwa akihudhuria ibada siku ya Jumapili, alisisitiza kuwa serikali yake haitavumilia maandamano yenye vurugu.

Alibainisha kuwa serikali yake iko tayari kushirikisha upinzani mradi tu gharama ya maisha ibaki nje ya mjadala.

Ruto aliteta kuwa manifesto yake ilikuwa imeweka kwa kina mpango wa kupunguza gharama ya maisha na kwamba apewe muda wa kuutekeleza.