Hospitali ya rufaa ya Moi yarudisha mkono uliokatwa na kutenganishwa kutoka kwa mwili

Mgonjwa huyo alikatwa mkono waker kutokana na vita vya kinyumbani lakini hospitali hiyo iliweka historia kwa mara ya kwanza kuurudisha mkono kwa mwili.

Muhtasari

• Ndani ya dakika 15 alipelekwa kwenye ukumbi wa upasuaji ambapo timu mbili za wanachama 13 zilipishana kazi.

Hospitali ya Moi.
Hospitali ya Moi.
Image: Facebook

Hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret imepiga hatua kubwa katika uwanja wa matibabu baada ya kufaulu kuurudisha kwa kuupachika mkono uliokuwa umekatwa.

Mgonjwa aliyerudishiwa mkono huo alikuwa mhanga wa vita vya nyumbani ambapo alikatwa mkono.

Kulingana na taarifa ya Jumapili, hospitali hiyo ilisema kuwa mgonjwa huyo aliyetambuliwa kama BK, 35, alikatwa mkono wake wa kushoto kwenye kifundo cha mkono kufuatia shambulio la kinyumbani siku ya Jumanne.

Kisha alipewa rufaa kutoka Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Sigowet, Kericho, na kufika katika Idara ya Dharura ya MTRH saa 4 asubuhi na kiungo kilichotenganishwa kilihifadhiwa kwenye sanduku baridi.

Ndani ya dakika 15 alipelekwa kwenye ukumbi wa upasuaji ambapo timu mbili za wanachama 13 zilipishana kazi ya kuunganisha tena kiungo hicho na mchakato ulikamilika kwa ufanisi saa tisa alasiri.

"Mgonjwa alirudishwa nyuma kwa mafanikio, alilazwa katika Kitengo cha Uangalizi wa baada ya matibabu (PACU) usiku kucha kisha Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) kwa ajili ya ufuatiliaji na kutiwa dawa ya IV ya Heparini. Alikamilisha uwekaji wa IV saa 48 baadaye siku ya Alhamisi tarehe 10/08/2023, kiungo kilichanika na ukarabati ulianza,” ilisoma sehemu ya taarifa hiyo kwa mujibu wa Citizen.

Siku ya Jumapili, BK alihamishwa kutoka ICU hadi Wodi ya Madaktari Mkuu wa Mifupa ambako ataendelea na ukaguzi na ukarabati wa kila siku.

Kenya ina madaktari bingwa watatu pekee wa upasuaji wa mikono, mmoja yuko Nairobi, mwingine Nakuru na Dk. Paul Mwangi kutoka MRTH, Citizen waliripoti.