Mume amuua mke wake miezi 5 tu baada ya kumuoa kama mke wa pili

Ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha miezi 5 tu ambayo mahakama ilielezwa kwamba kilikuwa ni kipindi cha mapito ya shubiri mke akifanywa chombo cha mazoezi ya ngumu na mumewe Ondara.

Muhtasari

• The Star wanaeleza kwamba Ondara alimuoa marehemu mkwe Gladys Munyenye kama mke wa pili mnamo 2011.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Mwanamume mmoja katika kauti ya Migori amehukumiwa upya jela kwa kupatikana na hatia ya kumuua mke wake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star, mwanamume huyo Hassan Ondara alimuuwa mke wake mwaka 2011 na kupatikana na hatia hiyo mahakamani mwaka 2016 ambapo alihukumiwa kifo.

Alikwenda katika mahakama ya rufaa akipinga hukumu huo lakini alipatwa na pigo la kudumu baada ya mahakama hiyo kudumisha uamuzi wa mahakama ya awali na kutaka faili za kesi yake kurudishwa kwenye mahakama ya juu ili kuhukumiwa upya tena.

Lakini ilianzaje?

The Star wanaeleza kwamba Ondara alimuoa marehemu mkwe Gladys Munyenye kama mke wa pili mnamo 2011.

Ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha miezi mitano tu ambayo mahakama ilielezwa kwamba  kilikuwa ni kipindi cha mapito ya shubiri kwa Munyenye ambaye aligeuzwa kuwa chombo cha mazoezi ya ngumu na mumewe Ondara.

Familia hiyo ilikuwa inaishi katika eneo la Kuria Magharibi, ikiwa ni kama kilomita moja hivi kutoka kwa kina Munyenye.

Siku moja, mwanawe Munyenye aliwashtukia wazazi wa Munyenye ambao ni bibi na babu kwa mtoto huyo akiwa peke yake na baada ya kuulizwa alisema kuwa babake ndiye alimsindikiza na kumfikisha karibu na nyumbani kabla ya kumuacha na kurudi.

Munyenye hakuonekana tena kwa wiki mbili na kipindi hicho chote mumewe alikuwa anauliza yu wapi mke wake lakini alikuwa anakwepa kujibu moja kwa moja, wakati mwingine akisema hajui.

Baada ya sku kadhaa, majirani walikuja kuupata mwili wa Munyenye ukiwa umezindikwa ndani ya shimo la maji chafu na ulikuwa umeharibika vibaya.

Ondara alitiwa mbaroni akiwa kama mshukiwa mkuu wa mauaji ya mke wake kwa kile kilisemekana kwamba alikuwa anajichanganya kwenye taarifa zake kuhusu uwepo wa mke wake Munyenye.

Februari 2016, alipatikana na hatia ya mauaji ya mkewe.