Hisia za Mutahi Ngunyi baada ya DP Gachagua kumwambia Raila anamuogopa

"Wacha Kalonzo na Kimani Ichung'wah wazungumze. Wewe, Ruto na mimi tunapaswa kukaa nje ya mazungumzo

Muhtasari
  • Hivyo alionya kuwa dhana zilizoibuliwa na Gachagua zinaweza kuzua utata kwa urahisi na kuibua mbegu ya mifarakano ndani ya Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.
Ngunyi atabiri kufeli kwa mazungumzo ya Azimio na Kenya Kwanza
Ngunyi atabiri kufeli kwa mazungumzo ya Azimio na Kenya Kwanza
Image: TWITTER

Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi amejibu matamshi ya naibu rais Rigathi Gachagua katika mazishi siku ya Ijumaa.

Huku akiwa mbele ya kiongozi wa muungano wa Azimio siku ya ijumaa naibu rais Gachagua alitoa sababu za kwa nini anaogopa kufanyika kwa hendisheki kati ya rais William Samoei Ruto na kinara wa upinzani.

Alisema baadhi ya sababu zinazomfanya aogope hendisheki ni kwamba hapo awali kati ya Raila na Uhuru kulisababisha uadui kati ya mkuu huyo wa zamani wa nchi na washirika wake wengi kutoka eneo la Mlima Kenya hivyo, wasingependa kuona mfano sawa.

“Nataka kukuambia leo kwa sababu upo hapa tunakuogopa.Hii ni kwa sababu ulimharibu mtoto wetu.Uhuru aliwahi kuwa rafiki yangu wa karibu, mimi nilikuwa PA wake lakini alipoungana na wewe alibadilika na sasa akataka nikamateni,” alisema Gachagua.

Akitumia akaunti yake rasmi ya Twitter, profesa Mutahi Ngunyi Alikubaliana na Naibu Rais akisema kuna ukweli katika taarifa hiyo.

"Mtu huyu Gachagua.. kuna kaukweli", alisema profesa Mutahi Ngunyi kwenye Twitter akinukuu kipande cha video cha taarifa ya Gachagua.

Gachagua na Raila walionekana kurushiana maneno makali kwenye mazishi, huku kinara huyo wa upinzani akikana madai ya gachagua kuwa alipatana na ruto.

Wakati wa hafla ya Ijumaa, Raila, kiongozi wa chama cha Azimio, alikanusha madai yaliyoenezwa na Gachagua kwamba alikutana kisiri na Rais William Ruto huko Mombasa na kuandaa makubaliano ambayo yaliwafungia nje vinara wenza wengine wa upinzani haswa Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Wiper.

Hivyo alionya kuwa dhana zilizoibuliwa na Gachagua zinaweza kuzua utata kwa urahisi na kuibua mbegu ya mifarakano ndani ya Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.

"Wacha Kalonzo na Kimani Ichung'wah wazungumze. Wewe, Ruto na mimi tunapaswa kukaa nje ya mazungumzo yanayoendelea. Hakuna ubaya kushiriki mazungumzo," Raila alimuonya Gachagua.

"Kila taifa lina matatizo, na Kenya si misamaha. Tumekabiliana na changamoto hapo awali, lakini tumezishinda kupitia mazungumzo ambayo yanaleta suluhu la amani," Raila alikariri msimamo wake wa kushirikisha serikali katika mazungumzo.