Kunuka mdomo husababisha upungufu wa nguvu za kiume - Daktari ashauri

Kulingana naye, kutunza vizuri meno na ufizi kunaweza kusaidia kuzuia shida za siku zijazo na uwezo wa mwanamume kusimamisha, na hivyo aliwashauri wanaume kutembelea daktari wa meno mara kwa mara.

Muhtasari

• Dk. Louisa Satekla alitambuliwa kama mwanafunzi bora zaidi wa meno katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, mwaka wa 2016.

Image: Maktaba

Daktari wa upasuaji wa meno wa Ghana Dk Louisa Satekla, ameacha mtu yeyote akishangaa na madai yake ya msingi ya utafiti kwamba wanaume walio na magonjwa ya fizi wanaweza kukosa nguvu za kiume.

Kulingana naye, kutunza vizuri meno na ufizi kunaweza kusaidia kuzuia shida za siku zijazo na uwezo wa mwanamume kusimamisha.

Dk. Louisa Satekla alitambuliwa kama mwanafunzi bora zaidi wa meno katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, mwaka wa 2016.

Daktari huyo aliyesherehekewa Zaidi alishiriki picha kwenye Instagram akielezea utafiti huo wake.

Alishiriki picha iliyo na kijisehemu kutoka kwa jarida la matibabu juu ya mada: Ushirika Kati ya Ugonjwa wa Muda Mrefu na Ukosefu wa Nguvu za Kuume: Uchunguzi wa Kudhibiti. "Je, wajua kwamba utafiti umeonyesha uhusiano kati ya magonjwa ya fizi na tatizo la kukosa nguvu za kiume? Ikiwa una baadhi ya dalili kama vile fizi kutokwa na damu, meno kulegea, ufizi kupungua au kuvimba, unapaswa kuonana na daktari wa meno HARAKA."

Chapisho la Louisa tangu wakati huo limevuta mazungumzo mengi kwenye mitandao ya kijamii.

Angalia kwenye kiungo hiki kujisomea maoni ya watu;