Hema Kubwa katikati ya uwanja wa Nyayo laibua hisia mtandaoni

Uwanja huo una uwezo wa kubeba takriban watu elfu arubaini na tano (45,000),

Muhtasari

• Picha za hema kubwa katikati mwa uwanja huo ziliwaacha wakenya na mswali mengi kuhusu ni nani aliyeihinisha hafla hiyo.

• Wengi walioguswa na picha hiyo walishangazwa nini maana ya tukio hilo

 

Nyayo Stadium/Facebook
Nyayo Stadium/Facebook

Wakenya katika miaka ya hivi majuzi, wamejihusisha na shughuli za michezo  kwani zimeonyesha  kuwa chanzo mbadala cha mapato yao.

Ikilinganishwa na miaka ya awali, wazazi wameonekana vilevile wakiunga mkono matamanio ya watoto wao ufuata talanta zao hasa katika michezo.

Vifaa vya michezo vimesalia kuwa na changamoto kwa wengi huku nchi ikikabiliwa na uhaba wa viwanja.

Uwanja wa Kimataifa wa Nyayo ambao unasimama kwa urefu jijini Nairobi,kwa muda murefu umekuwa kitovu cha hafla nyingi za michezo nchini Kenya.

Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba takriban watu elfu arubaini na tano (45,000),uliofunguliwa mmwaka wa 1983 umekua kituo cha kwenda pamoja na ule wa Kasarani.

Mnamo Jumatatu septemba 11, picha za hema kubwa katikati mwa uwanja huo ziliwaacha wakenya na mswali mengi kuhusu ni nani aliyeihinisha hafla hiyo.

Katika picha hizo,mamia ya viti vingeonekana vikiwa vimepangwa vyema kabla ya tukio lililoonkana kuwa la kanisa.

Wengi walioguswa na picha hiyo walishangazwa nini maana ya tukio hilo katika uwanja huo ambao umwahi kufungwa mara kadhaa ili kutoa muda kwa nyasi kuchipua.

Hata hivyo baadhi ya Wakenya hawakuona  suala lolote kuhusiana na tukio hilo wakishutumu wanaolalamikia unafiki. wakisema kuwa hawakulalamika wakati vyaa via kisiasa vilipofanya mikutano ya kisiasa viwanjani.

Sambamba  na umati mkubwa unotarajiwa kukanyaga eneo maridadi la kuchzea, nysi bila shka hazitapata mwanga wa kutosha wa jua kipindi cha tukio.

hizi ni baadhi ya hisia za wWakenya zilizochapishwa kwenye kurasa za mitandao kuhusiana na tukio hilo.

Mkenya anayetambulika kama George Makambi alisema;

"Huu ni ulaghai, ukosefu wa wazimu kabisa wa mawazo yenye maono kuhusu kampuni pekee iliyoidhinishwa na FIFA kuandaa michezo."

Shauriyako  makadara alighadhabishwa na kusema;

"Tatizo la Kenya ni kwamba, vifaa hvitumiki kwa malengo yaliyokusudiwa. Tunajifanya tunaelewa soka kwa kutazama Ligi ya uingereza lakini hatutambui kuwa sehemu muhimu ni ya uwanja,"

alexander Njiri naye aliongeza alifunga kwa kusema;

"wikendi iliyopita, tuliambiwa uwanja umefungwa kwa ukarabati, ni ukarabai mkubwa ulioje."