Kuku mkongwe zaidi duniani aliye hai ana umri wa miaka 21, atunukiwa cheti cha Guiness

Ndege huyo mwenye madoadoa ya kahawia ameishi na kuadhimisha mwaka wake wa 21 Mei 2023 huku akiwa bado ana afya njema na hai.

Muhtasari

• Kulingana na Marsi Parker Darwin, mzaliwa wa Michigan, alikuwa akijiandaa kutupa mayai yaliyokuwa yameoza kwenye kidimbwi cha mamba aliposikia mngurumo hafifu kutoka kwa moja ya yai.

Kuku aliyevunja rekodi ya Guiness.
Kuku aliyevunja rekodi ya Guiness.
Image: Screengrab

Shirika la kutambua rekodi za dunia Guiness wameripotiwa kumtambua na kumtunuku cheti kuku mmoja ambaye anatajwa kuwa mkongwe Zaidi duniani.

Kuku huyo aliyetambuliwa kwa jina Peanut ambaye anafugwa katika shamba moja na mkulima huko Michigan nchini Marekani alitunukiwa cheti cha Guiness kama kuku mwenye umri mkubwa Zaidi mwezi Januari mwaka huu akiwa na miaka 20 na siku 272.

Mapema wiki iliyopita, alisheherekewa tena akiwa na umri wa miaka 21 na siku 160.

Kinachovutia zaidi kuhusu maisha ya Kuku Peanut ni ukweli uliofunuliwa na mmiliki wake kwamba karibu atupe yai lililokuwa limembeba kuku huyo kama ifaranga.

Kulingana na Marsi Parker Darwin, mzaliwa wa Michigan, alikuwa akijiandaa kutupa mayai yaliyokuwa yameoza kwenye kidimbwi cha mamba aliposikia mngurumo hafifu kutoka kwa moja ya yai.

"Nilisikia mlio wa pili, na nikagundua kuwa kifaranga alikuwa hai na hakuonekana kuwa na jino la yai la kutoka kwenye ganda lake. Nilimtoa nje ya yai kwa upole, na kulikuwa na fujo hii ndogo, imeketi mkononi mwangu," alinukuliwa kusimulia wakati wa kutambulishwa rasmi kwa kuu wake na Guiness World Record.

Marsi anaripotiwa kusema kwamba aliamua kumpa kuku jina la ‘Peanut’ kwa sababu alikuwa mdogo sana wakati wa kuzaliwa na hakuwahi kukua zaidi ya uzani wa pauni moja, au karibu theluthi ya ukubwa wa kuku wengine wa shamba hilo.

Hata hivyo, kwa mshangao wake na mumewe, ndege huyo mwenye madoadoa ya kahawia ameishi na kuadhimisha mwaka wake wa 21 Mei 2023 huku akiwa bado ana afya njema na hai.

Rafiki mmoja alikuwa amependekeza kwa Marsi kuomba rekodi ya dunia ya Guinness kwa sababu alijua kuku anayeitwa Matilda, ambaye aliishi kwa miaka 14, rekodi ya karanga tayari ilikuwa imevunjwa wakati huo.