Lori lamuua mchuuzi wa ngono wakati akikimbilia pesa kutoka kwa mteja baada ya huduma

Kulingana na ripoti hizo, alianza kupigana na dereva wa teksi alipofika katika mtaa huo, akimtuhumu kufanya mapenzi naye na kukataa kulipia huduma hiyo adimu ya kusisimua mwili.

Muhtasari

• Wafanyabiashara wa ngono mara nyingi huhusika katika mapigano na wateja ambao wakati mwingine hukataa kulipa.

• Haya yanajiri huku nchini Kenya wachuuzi wa bidhaa hiyo katika kaunti ya Tana River miezi michache iliyopita wakitangaza kuongeza bei.

Makahaba (Picha; Maktaba)
Makahaba (Picha; Maktaba)

Mfanyabiashara wa ngono aligongwa na kuuawa kwa njia ya kusikitisha na lori lililokuwa likienda kasi katika barabara kuu ya nchini Ghana alipokuwa kwenye makabiliano ya kutaka malipo kutoka kwa anayedaiwa kuwa mteja ambaye alimhudumia, kituo cha Rainbow Radio kutoka nchini humo kimeripoti.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, marehemu aliyetambulika kwa jina moja tu – Anabel – alikuwa amekodisha teksi kuelekea sehemu hiyo alikoitwa na mteja wake wa mara kwa mara.

Kulingana na ripoti hizo, alianza kupigana na dereva wa teksi alipofika katika mtaa huo, akimtuhumu kufanya mapenzi naye na kukataa kulipia huduma hiyo adimu.

Dereva huyo alikanusha madai hayo na kudai kuwa ni mbinu tu ya kukwepa kulipa nauli ya teksi ya shilingi elfu moja. Kisha dereva akaondoka kwa kasi bila kulipa na kumwacha Anabel.

Walioshuhudia tukio hilo la majira ya usiku walisema kwamba wakati zogo hilo linaendelea, dereva aliingia kwa gari na kuondoka mbio na wakati Anabel anamkimbiza nyuma ndipo lori hilo lililokuwa kwa mwendo wa kasi lilimgonga na kumuua papo hapo.

Wafanyabiashara wa ngono mara nyingi huhusika katika mapigano na wateja ambao wakati mwingine hukataa kulipa baada ya kupewa huduma zao, na ilikuwa mojawapo ya matukio haya ambayo yalisababisha kifo cha huzuni cha Anabel.

Haya yanajiri huku nchini Kenya wachuuzi wa bidhaa hiyo katika kaunti ya Tana River miezi michache iliyopita wakitangaza kuongeza bei kwa kile walisema ni athari za kupitishwa kwa mswada wa fedha 2023 ambao ulifanya gharama ya maisha kupanda mara dufu.

Wachuuzi hao walinukuliwa na gazeti la Taifa Leo kwamba kuanzia mwezi jana bei ya huduma za ngono haitokuwa chini ya shilingi 500.

“Bei ya mipira (kondomu) imepanda, sawa na mahitaji mengine ya kimsingi kama vile chakula na maji. Wamiliki wa madanguro pia wanapandisha bei ya vyumba, sasa nasi inatubidi kupandisha,” waliambia Taifa Leo Dijitali.