Pasta akamatwa kwa kuendesha biashara ya watoto Kisii, aliwasafirisha kutoka Marsabit

Watoto hao 10 walipatikana wamefungiwa ndani ya chumba kimoja cha kulala wageni - loji - katika mji wa Kisii.

Muhtasari

• Makachero walivizia na kumtia mbaroni baada ya watoto hao 10 kupatikana wamefungiwa katika chumba kimoja cha kulala wageni – loji katika mji wa Kisii.

Mume amgonga mkewe kichwani kwa nyundo nzito kabla ya kujitia kitanzi.
Gari la polisi Mume amgonga mkewe kichwani kwa nyundo nzito kabla ya kujitia kitanzi.
Image: Screengrab//

Makachero wa DCI katika kauti ya Kisii wamemtia mbaroni mchungaji mmoja wa kanisa la kiadventista kwa madai ya kuendesha biashara ya ulanguzi wa watoto.

Kwa mujibu wa ripoti ya runinga ya Citizen, mchungaji huyo alikamatwa baada ya watoto 10 wneye kati ya umri wa miaka 5-10 kupatikana wamefungiwa katika chumba kimoja kinachodaiwa kukodishwa na mchungaji huyo.

Mchungaji huyo anadaiwa kwamba amekuwa akiendeshac biashaya hiyo ya kuwasafirisha watoto kutoka kaunti ya Marsabit hadi Kisii kwa madai ya kuwatafutia usaidizi lakini pindi wanapofika mikononi mwake, huwageuza kama bidhaa sokoni.

Makachero walivizia na kumtia mbaroni baada ya watoto hao 10 kupatikana wamefungiwa katika chumba kimoja cha kulala wageni – loji katika mji wa Kisii.

Idara ya uchunguzi ilisema kwamba mchungaji huyo hakuwa na barua yoyote kutoka kwa chifu wa wanakotoka watoto hao huko Marsabiti ili kumruhusu kuwa nao.

Watoto hao waliwekwa ndani ya gari la polisi pamoja na mchungaji huyo na kusafirishiwa hadi kituoni wanakosubiri uchunguzi kukamilika ili kubaini walikokuwa wanapelekwa watoto hao.

Hiki ni kisa kingine cha aibu ambacho kinamhusisha mtumizi wa Mungu katika msururu wa visa ambavyo vimekuwa vikitokea humu nchini vikiwahusisha wachungaji na wahubiri.