Mtaalamu wa wanyama mwenye miaka 52 aliyebaka mbwa 42 hadi kufa ahukumiwa

Inaaminika alianza kuudhi mwaka wa 2014 na amewatesa na kuwanyanyasa kingono zaidi ya mbwa 42 - wakiwemo wanyama wake vipenzi Ursa na Bolt.

Muhtasari

• Aliwadhulumu mbwa wake aina ya Swiss Shephards kwa karibu muongo mmoja kabla ya kuendeleza vitendo hivyo kwa wanyama wengine.

• Kulingana na ripoti alijipiga video katika kile alichokiita ‘chumba chake cha mateso’ akiwaumiza wanyama hao wasio na ulinzi hadi wengi wakafa.

 

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Mtaalamu wa wanyama amekiri katika orodha ya vitendo vya kuchukiza ikiwa ni pamoja na kubaka watoto wa mbwa na kuwatesa mbwa katika makazi ya wanyama nchini Australia.

Kwa mujibu wa majarida ya Uingereza anakotoka na Australia alikotenda unyama huo kwa wanyama, Mtaalamu wa mamba Adam Britton alitajwa kuwa mnyanyasaji wa wanyama siku ya Jumatatu (Septemba 25).

Alikiri mashtaka 60 yakiwemo mateso, ubakaji na mauaji ya mbwa wasiopungua 39.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 alikulia West Yorkshire kabla ya kuhamia Australia, ambapo vitendo vyake viovu vilitekelezwa.

Inaaminika alianza kuudhi mwaka wa 2014 na amewatesa na kuwanyanyasa kingono zaidi ya mbwa 42 - wakiwemo wanyama wake vipenzi Ursa na Bolt.

Kwa mujibu wa Daily Star, Britton, ambaye wakati mmoja alikuwa mgeni katika kipindi cha mtangazaji maarufu David Attenborough na kufanya kazi na BBC na National Geographic, aliwataja wanyama hao kama "wanasesere wake wa kingono" kabla ya kukamatwa Aprili 2022.

Aliwadhulumu mbwa wake aina ya Swiss Shephards kwa karibu muongo mmoja kabla ya kuendeleza vitendo hivyo kwa wanyama wengine.

Alihamia Gumtree Australia kutafuta wanyama zaidi wa kutesa au kuua. Britton alitumia soko la mtandaoni kutoa huduma kwa wamiliki wa wanyama vipenzi wanaohitaji mlezi wa mbwa kuwatazama wanyama wao vipenzi wanaposafiri au kufanya kazi, jarida hilo ilieleza Zaidi.

Kisha angejadiliana juu ya ulinzi wa mbwa. Ikiwa mmiliki aliomba masasisho juu ya mnyama, angebuni "hadithi ya uwongo" na kutuma picha za zamani.

Kulingana na ripoti alijipiga video katika kile alichokiita ‘chumba chake cha mateso’ akiwaumiza wanyama hao wasio na ulinzi hadi wengi wakafa.

Britton pia alishiriki video na picha zake akiwanyanyasa kingono wanyama mtandaoni.

Septemba 25, alikiri mashtaka 56 ya ukatili wa wanyama katika Mahakama ya Juu ya Wilaya ya Kaskazini. Pia alikiri makosa manne ya kupata na kusambaza nyenzo za unyanyasaji wa watoto.

Britton alishtakiwa mwaka jana, lakini jina lake lilibanwa na mahakama ili kuhakikisha usikivu wa vyombo vya habari hautapendelea mahakama dhidi yake.