Waliotumia iPhone 15 waibua malalamishi simu kutoa joto kali katika muda mchache wa matumizi

Mmoja alisema kwamba simu hiyo inapata halijoto ya zaidi ya 48°C ndani ya dakika 30 tu za matumizi, huku mwingine akisema kuiwasha tu dakika 2 ishapata joto la kutisha.

Muhtasari

• Ripoti hiyo ilidai kwamba Watumiaji wengi wamegundua iPhone 15 Pro yao inapata joto baada ya dakika chache - na mtu akilazimika kutumia barafu kuipunguza.

• Mwanablogu wa kiteknolojia wa China anayefahamika kwa jina Geekerwan alipata iPhone Pro inapata viwango vipya vya halijoto ndani ya dakika 30 pekee.

Nandy ampa mjakazi Iphone
Nandy ampa mjakazi Iphone
Image: Instagram

Ikiwa ni wiki moja baada ya kampuni ya Apple kuzindua msururu wa simu mpya za iPhone 15 pro, baadhi ya walionunua na kutumia simu hizo ghali sasa wameibua malalamishi na wasiwasi kuhusu utendakazi wa iPhone 15.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyokusanywa na Daily Mail ambapo walisema kwamba baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wameonesha kutamaushwa kwao na pia kujuta kumwaga hela ndefu kupata simu hizo ghali ambazo sasa wanadai zina mapungufu si haba.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Mtumiaji mmoja wa X, @GeekmanGreg, alisema: 'Nina hisia kwamba iPhone 15 itaishia kuwa kosa kubwa la Apple katika historia kwao.'

Ripoti hiyo ilidai kwamba Watumiaji wengi wamegundua iPhone 15 Pro yao inapata joto baada ya dakika chache - na mtu akilazimika kutumia barafu kuipunguza.

Mtumiaji mmoja alienda kwa X kusema: 'Titanium ya asili ya iPhone 15 Pro inakuwa moto sana, hivi kwamba inakuwa ngumu kushikilia. Inapata joto baada ya kiwambo kuwashwa kwa dakika 2 tu au mtu anapofungua reels za mitandaoni kwa dakika 8-10.”

Watumiaji kwenye Support Community ya mtandaoni ya Apple pia walishiriki kwamba wamekuwa na changamoto sawa na hiyo, Daily Mail walisema.

Mwanablogu wa kiteknolojia wa China anayefahamika kwa jina Geekerwan alipata iPhone Pro inapata viwango vipya vya halijoto ndani ya dakika 30 pekee.

'Joto la skrini ya iPhone 15 Pro liliweka rekodi mpya katika matumizi yangu ya iPhone, kufikia 48°C,' alisema kwenye video iliyotumwa kwenye YouTube.

Image: x