Baba amekuwa mtu wangu-Rais Ruto awaambia wakazi wa Homabay

Alikuwa mmoja wa watu sita waliounda bodi kuu ya maamuzi ya chama cha ODM inayoitwa Pentagon.

Muhtasari
  • Ruto, pamoja na waasi wengine wa ODM walihama chama kinachoongozwa na Raila Odinga kabla ya 2013.

Rais William Ruto ametoa wito wa umoja kati ya viongozi katika migawanyiko yote ya kisiasa.

Akizungumza mjini Homa Bay Jumamosi, Ruto alipokuwa akijibu matamshi ya Gavana Gladys Wanga, alisema wakati mmoja alikuwa sehemu ya kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Hata aliendelea na kufichua kuwa kwa sasa, Raila ni 'mtu' wake.

"Si ata nyinyi mnajua nilikuwa mtu wa baba. Ili raila aitwe former Prime Minister , hiyo kiti nani alimtafutia. Si ni mimi na watu wengine,"Ruto said.

"Sasa siku ile nilikuwa mtu wa baba, lakini sasa mimi ni rais, baba amekuwa mtu wangu," aliongeza.

Rais alikuwa akijibu matamshi ya Gavana Wanga kwamba watu wa Homa Bay akiwemo yeye ni wafuasi wa Raila.

Ruto alikuwa kiongozi wa kabila la Wakalenjin katika chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na alihusika na kampeni za chama hicho katika Mkoa wa Bonde la Ufa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2007.

Alikuwa mmoja wa watu sita waliounda bodi kuu ya maamuzi ya chama cha ODM inayoitwa Pentagon.

Wengine ni marehemu Joseph Njaga, aliyekuwa Waziri wa Utalii Najib Balala, Raila, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri na Musalia Mudavadi.

Ruto, pamoja na waasi wengine wa ODM walihama chama kinachoongozwa na Raila Odinga kabla ya 2013.

Hata hivyo, Julai 29, 2023 Chifu wa Upinzani alikutana na Rais Ruto katika mkutano.

Hii ilikuwa mara ya kwanza wawili hao kukutana kisiri baada ya uchaguzi.

Siku ya Jumatano, Raila Odinga alifichua maelezo ya mkutano huo wa siri ambao ulihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo mnamo Julai 29.

Raila alifichua kuwa rais huyo wa zamani wa Nigeria aliketi katikati wakati wa mkutano huo ambao alisema walikubaliana jinsi ya kushughulikia masuala muhimu ambayo yalikuwa yameibuliwa.

"Tulikuwa watatu tu chumbani. Kulikuwa na Obasanjo, Ruto, na mimi mwenyewe. Obasanjo alikuwa amekaa katikati, Ruto pale, na mimi nilikuwa hapa katika chumba kimoja. Ilifanyika si katika nyumba ya serikali lakini katika majengo mengine. Raila alisema wakati wa mahojiano.