Raila anapaswa kunipigia kura 2027-Rais Ruto

Alikariri wito wake wa umoja wa kitaifa, akiwataka wakaazi kutazama zaidi ya tofauti za kisiasa.

Muhtasari
  • Aliendelea kusema kuwa aliidhinisha azma ya Raila Odinga kuwania urais mwaka wa 2007 na sasa anatazamia kuungwa mkono katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Rais William Ruto sasa anasema kuwa kio0ngozi wa muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga ana deni lake la kisiasa.

Ruto alidai kuwa Raila Odinga anadaiwa uungwaji mkono wa kisiasa kwa sababu ya sehemu yake katika uteuzi wa waziri mkuu huyo wa zamani alipoanza siku ya pili ya ziara ya siku nne ya maendeleo katika eneo la Luo-Nyanza.

"Nilikuwa mfuasi wa Raila. Ili aweze kutajwa leo kuwa Waziri Mkuu wa zamani, mimi ndiye niliyemsaidia kumweka ofisini," alisema katika hotuba yake kwa wakazi wa Kaunti ya Homabay jana.

Aliendelea kusema kuwa aliidhinisha azma ya Raila Odinga kuwania urais mwaka wa 2007 na sasa anatazamia kuungwa mkono katika uchaguzi mkuu wa 2027.

“Nilimpigia kura ‘Agwambo’ (Raila Odinga) na hajawahi kunipigia kura. Sasa nitasubiri kura yake katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 kwa sababu ikiwa hatagombea, nitagombea pamoja na Kalonzo Musyoka,” Ruto alisema.

"Nilipata kiti cha urais nilichowania, na sasa natoa wito wa umoja ili kuipeleka Kenya mbele."

Alikariri wito wake wa umoja wa kitaifa, akiwataka wakaazi kutazama zaidi ya tofauti za kisiasa.

"Usihoji ni kwa nini nilifika kaunti ya Homabay, ingawa sikupokea kura kutoka kwenu. Homabay ni sehemu muhimu ya Kenya, na ninaahidi kufanya kazi kwa ajili ya kuboresha taifa zima," alisema.