Watahiniwa wa Form 4 wakamatwa kwa kuchapa wanafunzi wengine kama ishara ya kwaheri

Waliokamatwa ni vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 19 na ambao wote ni watahiniwa wanaotarajia kuketi mitihani yao ya kitaifa siku chache zijazo.

Muhtasari

• Inasemekana imekuwa ni utamaduni shuleni hapo, ambapo wanafunzi wa kidato cha nne hupigwa na wanafunzi kutoka madarasa mengine kama ishara ya kuwaaga.

• Hata hivyo, safari hii wanasemekana kujipanga na kuwashambulia wenzao na kuzua vurugu shuleni.

Pingu
Image: Radio Jambo

Vurugu zilirupotiwa kutokea katika shule moja nchin iUganda baada ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu kulalamikia kuchapwa viboko na wenzao wa kidato cha nne wanaokaribia kufanya mitihani ya kitaifa kama njia moja ya kile wanasema ni kuwaambia kwaheri.

Kwa mujibu wa jarida moja kutoka nchini humo Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika shuleni humo na kutuliza hali kwa kuwakamata watahiniwa 7 ambao walishukiwa kuongoza vurugu hizo za kuwatia mijeledi wananfunzi wenzao.

Waliokamatwa ni vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 19 na ambao wote ni watahiniwa wanaotarajia kuketi mitihani yao ya kitaifa siku chache zijazo.

Inasemekana imekuwa ni utamaduni shuleni hapo, ambapo wanafunzi wa kidato cha nne hupigwa na wanafunzi kutoka sehemu nyingine za madarasa, ikiwa ni njia ya kuwaaga.

Hata hivyo, wakati huu, watahiniwa wa kidato cha nne waandamizi, wanasemekana kujipanga na kuwashambulia wanafunzi wa madarasa mengine, na hivyo kuzua mapigano makali kati ya wanafunzi ndani ya shule.

Kulingana na msemaji wa polisi nchini humo, Fred Enanga, polisi kutoka walijibu na kurejesha akili katika shule hiyo.

Aidha msemaji huyo alibainisha kuwa viongozi saba wa mapigano hayo wametambuliwa na kukamatwa.

Katika mapigano hayo wanafunzi wawili walipata majeraha na kukimbizwa katika hospitali kwa matibabu.