Mashabiki wa Lupita Nyong'o wamuunga mkono baada ya kuachana na Selema Masekela

‘’Ninajikuta katika msimu wa kuvunjika moyo kwasababu ya penzi’’, aliandika bila kumtaja mtu yeyote.

Muhtasari
  • Nyongo alisema kwenye mtandao wa Instagram , akisema kwamba alitakuwa kufichua ukweli wake wa kibinnafsi.
Selema Masekele na Lupita Nyong'o
Selema Masekele na Lupita Nyong'o
Image: Hisani

Mashabiki wa mwigizaji wa Hollywood na rai awa Kenya Lupita Nyongowamemtetea baada ya kufichua kwamba ameachana na mpenzi wake kutoka Marekani na mtangazaji wa runinga Selema Masekela.

Nyongo alisema kwenye mtandao wa Instagram , akisema kwamba alitakuwa kufichua ukweli wake wa kibinnafsi.

‘’Ninajikuta katika msimu wa kuvunjika moyo kwasababu ya penzi’’, aliandika bila kumtaja mtu yeyote.

Masekela hajasema lolote na amefunga eneo la maono katika akaunti yake ya Instagram.

Nyong’o , mwigizaji wa Hollywood ambaye aliweka historia2014 kama Mkenya wa kwanza kushinda tuzo ya Oscarna Mwafrika wa pili kushinda tuzo hiyobaada ya muigizaji wa Afrika Kusini Charlize Theron , aliuweka uhusiano wake na Masekela hadharanimwezi Disemba mwaka uliopita.

‘Tulipendana tu!’ , Nyongo aliandika chini ya kanda ya video akizungumzia kuhusu uhusiano wao , ambayo ameifuta.

Selema , mwana wa gwiji wa muziki wa Jazz Hugh Masekela, pia alizungumzia kuhusu Nyong’okatika chapisho lake jingine.

’Mioyo yetu imekubaliana’’ . Mpenzi wangu Lupita Nyongo, alisema.

Katika chapisho lake baada ya kuachana , Nyong’o aliandika kwamba alitaka kujitenga na mtu ambaye hawezi kumuamini tena na kwamba mapenzi yake yalifutwa na udanganyifu