Mungu anisamehe kwa matusi - Ujumbe wa Sonko kwa Uhuru Kenyatta

Sonko aliendelea kuomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa matusi aliyomtusi Kenyatta siku za nyuma.

Muhtasari
  • "Nimemzawadia keki, kadi na vinywaji bora kama ishara ya kukosa siku za furaha tulizokuwa nazo kabla na baada ya kuwa rais," sehemu ya taarifa hiyo ilisema.

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko ameungana na Wakenya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Katika ujumbe wake kwenye jukwaa la X mnamo Jumamosi, Oktoba 28, Sonko alifichua kwamba alimzawadia Rais huyo wa zamani keki, kadi na vinywaji bora kama ishara ya kukosa siku za furaha.

"Imeandikwa katika kitabu cha Mathayo 5:43. "Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa." Ninamsherehekea Rais wa zamani, Uhuru Muigai Kenyatta. Bwana Mwema ampe afya njema na maisha marefu anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 62.

"Nimemzawadia keki, kadi na vinywaji bora kama ishara ya kukosa siku za furaha tulizokuwa nazo kabla na baada ya kuwa rais," sehemu ya taarifa hiyo ilisema.

Sonko aliendelea kuomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa matusi aliyomtusi Kenyatta siku za nyuma.

"Heri ya siku yako ya kuzaliwa ndugu yangu, na mwaka wako wa nyongeza ukuletee furaha. Mungu anisamehe kwa matusi, maneno yasiyofaa na chochote nilichosema kukuchochea ulipize kisasi. Pia nimekusamehe makosa na mateso yote. Uishi maisha marefu. Mungu akubariki wewe na familia yako," alisema.

Wakenya walimsherehekea Rais huyo wa zamani mnamo Alhamisi, Oktoba 26 wakati wa siku yake ya kuzaliwa huku Kenyatta akiongoza vilivyovuma kwenye jukwaa la X.

Rais huyo wa zamani alipigiwa simu na mtangazaji wa Kameme ambaye alimtakia heri ya siku ya kuzaliwa huku mtangazaji huyo akiomba kibao cha 'I got you babe' ya UB40.