Jamaa achoma vyeti vyake vyote baada ya kukosa kazi miaka 13 tangia kufuzu chuo kikuu

Jamaa huyo kwa kutamauka alisema kwamba licha ya kuwa na masomo hadi chuo kikuu, amekuwa akifanya kazi za ngazi za chini, akisimamiwa na watu ambao hawakusoma wala hawajui kuandika.

Muhtasari

• Aliongeza kuwa atamshauri mtu yeyote aende kujifunza kazi sasa badala ya kwenda Chuo Kikuu huku akibeza vyeti vinavyotolewa na taasisi za juu.

Mhitimu akichoma vyeti.
Mhitimu akichoma vyeti.
Image: Instagram

Hisia nyingi zimezuka kufuatia video inayovuma ambapo mhitimu wa Chuo Kikuu kutoka Nigeria alichoma vyeti vyake kufuatia kutoweza kupata kazi nzuri baada ya kumaliza masomo.

Mhitimu aliyekatishwa tamaa wa Chuo Kikuu alichoma vyeti vyake vyote kuanzia digrii yake, hadi cheti chake cha shule ya msingi miongoni mwa vingine baada ya kukosa kupata kazi nzuri miaka 13 baada ya kumaliza shule.

Katika video hiyo, mhitimu huyo raia wa Nigeria mwenye umri wa makamo anaeleza kusikitishwa na hali ya mambo nchini huku akiongeza kuwa anaburuza kazi kwa watu wasiojua kusoma na kuandika licha ya kuwa ni mhitimu wa Chuo Kikuu.

Kulingana na mhitimu huyo wa Chuo Kikuu, hakuna umuhimu wowote wa kuwa na vyeti kwani si lolote bali ni kupoteza muda.

Akiongeza sababu zaidi iliyomfanya aamue kuchoma cheti chake, mwanaume huyo alisema kuwa nchi zingine nje ya nchi yake hazikubali hata digrii za Nigeria na itabidi mtu aishie kujifunza kitu.

Sauti ilisikika kwa nyuma ikimwambia mhitimu wa Chuo Kikuu asichome cheti chake, lakini alikataa kwa vile alidai hakuna sababu ya kuwa na vyeti vyote kwa sababu hakuna tofauti kati ya wanaojua kusoma na kuandika na wasiojua kusoma na kuandika nchini Nigeria.

Aliongeza kuwa atamshauri mtu yeyote aende kujifunza kazi sasa badala ya kwenda Chuo Kikuu huku akibeza vyeti vinavyotolewa na taasisi za juu.

Pia alibainisha wakati akichoma vyeti kuwa kazi anayokaribia kuipata sasa ni ya rafiki yake ambaye hakwenda Chuo Kikuu lakini wote walisoma shule moja ya msingi.

Tazama video hapa chini;