Wacheni wawekezaji wafanye kazi-Raila awaambia wanasiasa kuhusu kampuni ya Mumias

"Mimi sitaki tena mambo ya Mumias makelele...yule investor ako hapo kwa sasa apewe nafasi afanye kazi

Muhtasari
  • Alitumia jukwaa kutoa wito kwa viongozi wa Magharibi mwa Kenya kukomesha siasa za mpango wa ufufuaji wa Mumias akisema wakulima wamekuwa wakipata faida tangu kiwanda hicho kusimama.
Raila Odinga
Raila Odinga
Image: Facebook

Kiongozi wa Chama cha Muungano wa Azimio-One Kenya Raila Odinga anawataka wanasiasa kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya kuachana na siasa za Mumias na kuruhusu wawekezaji kurejesha uhai katika Kampuni ya Sukari ya Mumias.

Odinga ambaye alikuwa Matungu, Kaunti ya Kakamega kwa mazishi ya MCA mteule Godliver Omondi alitoa imani kuwa mwekezaji huyo mpya atabadilisha sekta ya sukari Magharibi mwa Kenya ambayo imekuwa ikipiga magoti.

Alitumia jukwaa kutoa wito kwa viongozi wa Magharibi mwa Kenya kukomesha siasa za mpango wa ufufuaji wa Mumias akisema wakulima wamekuwa wakipata faida tangu kiwanda hicho kusimama.

"Mimi sitaki tena mambo ya Mumias makelele...yule investor ako hapo kwa sasa apewe nafasi afanye kazi.....mimi ni engineer na nimeenda kwa kiwanda hicho nanajua kazi ile mbaya pale," Odinga said.

Rais William Ruto katika muda wa miezi miwili iliyopita amekuwa na vita kali dhidi ya kile alichokiita makampuni ya sukari ambayo yamekuwa yakiwadhulumu wakulima. Hii ilisababisha kuondolewa kwa kesi dhidi ya Kampuni ya Sukari ya Mumias zilizokuwa zimewasilishwa na mfanyabiashara Jaswant Rai.

Odinga ameonya Ukanda wa Magharibi mwa Kenya kuwa kushindwa kufanya kazi na mwekezaji wa sasa kutazidi kuwazamisha wakulima wa Kanda ya Magharibi katika umaskini zaidi.

“Mkiendelea na makelele mtakaa miaka kumi bila kuuza miwa yenu na ni wakulima ndio wataumia...kwa hivyo mimi kama kiongozi wenu nawaomba muache siasa mbaya ya Mumias mfanye kazi wakulima wafaidike,” alisema Odinga.