Oscar Sudi amsherehekea binti yake kwa kupata digrii ya Masters kutoka chuo cha UK

Haya yanajiri wakati ambapo kiongozi huyo amekuwa akikumbwa na kesi mahakamani kuhusiana na uhalali wa vyeti vyake vya masomo.

Muhtasari

• Haya yanajiri wakati ambapo kiongozi huyo amekuwa akikumbwa na kesi mahakamani kuhusiana na uhalali wa vyeti vyake vya masomo.

Oscar Sudi
Oscar Sudi
Image: X

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ni baba mwenye furaha baada ya bintiye kufuzu kutoka chuo kimoja nchini Uingereza na shahada ya uzamili.

Kupitia kurasa zake mitandaoni, mbunge huyo anayetajwa kuwa hana elimu ya kihivyo alipakia mfululizo wa picha za sherehe ambayo waliandaa nyumbani Kapseret kumkaribisha binti huyo baada ya kufuzu kutoka chuo cha Kent, nchini Uingereza.

Sudi kwa kujihisi fahari ya baba, hakusita kufichua kuwa bintiye alifuzu katika kitivo cha masuala ya usimamizi wa fedha.

“Imekuwa safari ngumu kwa binti yangu Faith Chemutai katika maisha yake yote ya masomo. Amehitimu tu Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Kent, Canterbury, Uingereza. Leo tunaposherehekea mafanikio yake nyumbani, Kapseret,” aliandika kwenye picha hizo.

Habari zingine ambazo hazijathibitika hata hivyo zinadai kwamba Sudi alimpa mwanawe zawadi ya gari pamoja na nyumba jijini Nairobi kwa jitihada zake masomoni.

Kaitka hafla hiyo ya shukrani, viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo gavana wa Uasin Gishu lakini pia mwanariadha mashuhuri Eliud Kipchoge.

Haya yanajiri wakati ambapo kiongozi huyo amekuwa akikumbwa na kesi mahakamani kuhusiana na uhalali wa vyeti vyake vya masomo.