Mke agundua mumewe amekuwa akimbaka kwa miaka 9 kila alipokuwa amepoteza fahamu

Mwanamke huyo aliongeza kuwa alihisi kuwa alikuwa ameolewa na mtu asiyemjua, ambaye ndiye aliyemfanyia 'unyanyasaji mbaya na wa jeuri zaidi'.

Muhtasari

• Tangu ugunduzi huo wa kushangaza, alisema kuwa amefuta kumbukumbu zote za mwanamume huyo kutoka kwa familia yake.

• "Lakini siwezi kufuta maumivu, fedheha na udhalilishaji alionipitia," alisema.

• Unyanyasaji huo ulitokea katika nyumba ya familia kwa tarehe zisizojulikana kati ya Januari 2005 na Septemba 2014.

Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Mwanamke mmoja nchini Ireland alipigwa na butwaa mahakamani baada ya mumewe kukiri kwa mashtaka ya kuwa amekuwa akimbaka kwa kutumia vitu vya jikoni kwa Zaidi ya miaka 9, kila mara alipokuwa anapoteza fahamu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kutamausha iliyopeperushwa jarida la Irish Examiner, mwanamume huyo alipatikana na hatia ya kumdhulumu mkewe na kuhukumiwa kifungo cha miaka 11 jela.

Mwanamume huyo wa Dublin, mwenye umri wa miaka 49, alipatikana na mahakama mwezi uliopita na hatia ya makosa 11 ya kumnyanyasa mkewe kingono kati ya Januari 2005 na Septemba 2014.

Bw Jaji Paul Burns alimhukumu kifungo cha miaka 12, lakini akasimamisha mwaka wa mwisho kwa masharti kadhaa, ikiwa ni pamoja na mwanamume huyo kushiriki katika kozi ya kujamiiana na ridhaa, gazeti la Irish Examiner linaripoti Zaidi.

Hakimu huyo alisema ilikuwa vigumu kueleza yale ambayo mwathiriwa amepitia, kwa kujua kuhusu unyanyasaji huo alipogundua 'picha hizo za kudhalilisha na kuchafua utu' na wakati wa kesi, picha hizo zilipoonyeshwa kwa majaji.

Alipitia kesi hizi 'kwa ujasiri mkubwa na heshima,' jaji aliongeza.

Haya yanajiri baada ya mkewe kushutumu 'mawazo yake ya mgonjwa' kwa kauli ya kuhuzunisha.

Mwanamke huyo aliyejawa na hofu aligundua mume wake wa zaidi ya miaka 20 amekuwa akimbaka mara kwa mara akiwa amelala baada ya kupata 'picha hizo za kutisha' kwenye kompyuta yake.

Unyanyasaji huo ulitokea katika nyumba ya familia kwa tarehe zisizojulikana kati ya Januari 2005 na Septemba 2014.

Mwanamume huyo hata hivyo, aliendelea kudumisha kutokuwa na hatia, lakini hakimu alisema ubakaji wake wa mara kwa mara unajumuisha 'ukiukaji mkubwa wa uaminifu wa kawaida kati ya wanandoa', jarida hilo lilieleza.

Katika taarifa yake ya athari ya mwathiriwa, ambayo ilisomwa na mmoja wa wachunguzi wa kesi hiyo, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 alisema hakujua kwamba mumewe alikuwa 'katika ponografia', achilia mbali kumtumia kwa 'mawazo yake mabaya ya kujiridhisha kimwili'.

Tangu ugunduzi huo wa kushangaza, alisema kuwa amefuta kumbukumbu zote za mwanamume huyo kutoka kwa familia yake. "Lakini siwezi kufuta maumivu, fedheha na udhalilishaji alionipitia," alisema.

Mwanamke huyo aliongeza kuwa alihisi kuwa alikuwa ameolewa na mtu asiyemjua, ambaye ndiye aliyemfanyia 'unyanyasaji mbaya na wa jeuri zaidi'.