Mrembo 'aliyeolewa' na mdoli adai maisha ya ndoa ni magumu baada ya kupata 'mapacha'

Meirivone Rocha Moraes, 37, kutoka Brazil, aliwahi kugonga vichwa vya habari kwa kufichua undani wa uhusiano wake na Marcelo, mdoli wa viraka na watoto wao wa viraka.

Muhtasari

• 'Na hata ninapokuwa nimechoka, yeye [mume wangu] hunisaidia kuoga, kula na kulala.'

• Alisema kwamba wenzi hao hupata shangwe kwa kuwa na nyumba yao iliyojaa upendo, kicheko, na watoto midoli.

Meirivone Rocha Moraes, mwanamke aliyefunga ndoa na mdoli wa viraka.
Meirivone Rocha Moraes, mwanamke aliyefunga ndoa na mdoli wa viraka.
Image: Instagram//Meirivone Rocha Moraes

Mwanamke 'aliyeolewa' na mwanasesere wa viraka ambaye anashiriki 'watoto' watatu wa wanasesere amesema maisha ya familia yao ni 'magumu'.

Meirivone Rocha Moraes, 37, kutoka Brazil, aliwahi kugonga vichwa vya habari kwa kufichua undani wa uhusiano wake na Marcelo, mdoli wa viraka na watoto wao wa viraka, akiwemo Marcelinho wa mwaka mmoja, na mapacha wawili 'wachanga' binti, Marcela na Emilia.

Lakini kuwa na familia kamili ni changamoto kwa mama wa watoto watatu, ambaye anaeleza kuwa wanashiriki majukumu ya mzazi.

"Ni ngumu kusema kwa sababu kila kitu kiko katika dozi mbili [kwa kuwa tuna mapacha]," Meirivone alisema.’

'Siyo rahisi lakini wakati huo huo, mimi hupata hisia kila dakika, kila sekunde.

'Katika maisha ya kila siku, mimi na Marcelo tuna kazi nyingi na watoto wachanga, pamoja na kutunza mtoto wetu wa kwanza.’

'Na hata ninapokuwa nimechoka, yeye [mume wangu] hunisaidia kuoga, kula na kulala.'

Alisema kwamba wenzi hao hupata shangwe kwa kuwa na nyumba yao iliyojaa upendo, kicheko, na watoto midoli.

Walakini, Marcelo amepata bei ya kuwa na familia kubwa yenye mafadhaiko.

Alisema: 'Gharama zinaongezeka na analazimika kulipia chakula, nguo, kodi, maji, umeme na dawa. Kwa hiyo amekuwa na wasiwasi kidogo kuhusu kumudu bili.’

"Lakini licha ya wasiwasi wake, siku zote alikuwa na ndoto ya kuwa na familia na watoto, hivyo hii ndiyo yote aliyowahi kutamani."

Meirivone aliongeza: 'Ndoto yangu sasa ni kumiliki nyumba yangu mwenyewe. Tangu harusi yetu mnamo 2018, nimekuwa nikijivinjari mtandaoni kila siku, sitakata tamaa.'

Uhusiano wa wanandoa hao umekuwa na misukosuko mingi katika miaka miwili iliyopita, kutoka kwa uvumi wa kuchepuka hadi utekaji nyara.