Video ya Uhuru na Ruto wakijaribu kutokutanisha macho wakiketi kwa ukaribu yazua gumzo

Hata baada ya kuchaguliwa, Ruto amekuwa akilaumu hali mbaya ya kiuchumi inayolikumba taifa kwa utawala wa mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta.

Muhtasari

• Lakini pia kumeibuka video ambayo imeonesha jinsi wawili hao walikuwa wameketi kuhudhuria hafla hiyo ya kiserikali.

Ruto n Uhuru
Ruto n Uhuru
Image: screengrab

Rais William Ruto na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza tangu mwaka jana alipoapishwa, walikutana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC katika hafla ya kitaifa ya kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi.

Picha kutoka kwa hafla hiyo ambayo imewafurahisha wengi ni baada ya wawili hao kuonekana wakisalikiaka kwa furaha huku kila mmoja akiwa anatabasamu.

Lakini pia kumeibuka video ambayo imeonesha jinsi wawili hao walikuwa wameketi kuhudhuria hafla hiyo ya kiserikali.

Katika picha hiyo, Uhuru Kenyatta alikuwa ameketi mita chache kutoka kwa Rutok nyuma yake huku kila mmoja akiwa bize karibu kujitahidi kutogeuza jicho lake kumuangalia mwenzake.

Video hiyo imevutia maoni kinzani katika mtandao wa X ambapo baadhi wameichambua kwa jinsi wawili hao kila mmoja alikuwa hataki kabisa kujua uwepo wa mwenzake licha ya kuwa walikuwa marafiki wakubwa miaka ya nyuma.

Uhuru alihudhuria hafla hiyo kama Mwezeshaji wa Mchakato wa Amani wa Nairobi unaoongozwa na EAC.

Waliketi karibu na kila mmoja wakati wa kuapishwa kwa Rais Ruto Kasarani mnamo Septemba 13, 2022.

 Wawili hao wamekuwa wakihasimiana tangu kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, ambapo Ruto alikuwa amejitenga na mambo mengi ya serikali ya Kenyatta ambayo alikuwa kama naibu rais.

Hata baada ya kuchaguliwa, Ruto amekuwa akilaumu hali mbaya ya kiuchumi inayolikumba taifa kwa utawala wa mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta.