Askofu Margaret Wanjiru adai polisi vijana walimgusa kwenye mapaja kanisa likipomolewa

“...huyu Margaret Wanjiru ambaye alipigwa, vazi langu kuinuliwa juu na vijana wadogo ambao ni polisi, waligusa mapaja yangu, mimi, mwanamke wa Mungu…”

Muhtasari

•"Mlikwenda kumtafuta Benny Hinn kutoka Marekani, mtanitafuta na sisongi hata kidogo, siendi mahali, nitakuwepo hapa" aliwaambia Ruto na Gachagua.

Margaret Wanjiru
Margaret Wanjiru
Image: Facebook

Askofu Margaret Wanjiru wa kanisa la Jesus Is Alive Ministries – JIAM – amezua madai makali dhiti ya polisi, akidai kwamba walimnyanyasa wakati wa mzozo wa kujaribu kuzuia ubomozi wa kanisa lake eneo la katikati mwa jiji la Nairobi.

Akizungumza kutoka kwenye kiti cha magurudumu akiwa amezungukwa na wahubiri wenzake, Wanjiru alidai kwamba maafisa wa polisi vijana walimshika visivyo kwenye sehemu za mapaja baada ya kuinua vazi lake juu, jambo ambalo alilikashifu na kuishtumu serikali kwa madhira yake.

Wanjiru aliwaahidi rais Ruto na naibu wake Margaret Wanjiru kwamba urafiki wao umeshakatika na siku moja watamtafuta kama ambavyo walienda kumtafuta mwinjilisti Benny Hinn kutoka Marekani.

“Sasa achene niwaambie kitu Fulani, rais wangu na naibu rais wangu, kuanzia leo, huyu Margaret Wanjiru ambaye alipigwa, vazi langu kuinuliwa juu na vijana wadogo ambao ni polisi, waligusa mapaja yangu, mimi, mwanamke wa Mungu…”

“Ninataka kutoa ahadi tamu kwenu, mtanitafuta. Mlikwenda kumtafuta Benny Hinn kutoka Marekani, mtanitafuta na sisongi hata kidogo, siendi mahali, nitakuwepo hapa. Mmeanza vita ambavyo hamtaviweza. Hii iko katika orodha ya mbinguni,” alisema.

Wanjiru alidai kwamba serikali inajificha nyuma ya MD wa Railways akidai kwamba anaisikitikia familia yake pamoja na ya viongozi wa serikali husika kwani machozi ambayo alilia tangu juzi hayatakauka bure, lazima watayalipia.