Roysambu: Kijana wa miaka 32 afariki baada ya kudaiwa kunywa pombe ya ‘Rest In Peace’

Kijana huyo alianza kutapika damu baada ya kunywa pombe hiyo yenye jina la chapa ‘Rest in Peace’ na alifariki muda mfupi baadaye Machi 4, 2024.

Muhtasari

• Muchina alizikwa Gatundu Kusini, na Wakenya, katika wadhifa huo, walitoa wito kwa serikali kupeleka hatua kali katika kukabiliana na aina hii ya pombe.

Rip
Rip
Image: HISANI

Familia moja katika mji wa Roysambu viungaji mwa jiji la Nairobi inaomboleza baada ya mpendwa wao kufariki baada ya kudaiwa kunywa moja ya pombe hatari.

Kijana huyo kwa jina Francis Muchina mwenye umri wa miaka 32 anasemekana kufariki siku chache zilizopita, baada ya kuugua muda mfupi baada ya unywaji wa pombe hiyo eneo la Rosyambu, Nairobi.

Kulingana na habari iliyosambazwa na mwandishi wa habari wa Inooro TV Simon Kibe, Muchina, anayejulikana pia kama Kevo, alianza kutapika damu baada ya kunywa pombe hiyo yenye jina la chapa ‘Rest in Peace’ na alifariki muda mfupi baadaye Machi 4, 2024.

Kibe pia alieleza uchungu ambao familia hiyo imekuwa ikikumbana nao tangu kumpoteza mwana wao katika kisa hicho kibaya.

"Kuna pombe mbaya inayojulikana kwa jina la 'Rest in Peace' inauzwa Roysambu. Bibi huyu atamzika mtoto wake kesho baada ya kunywa pombe hiyo. Inauma sana," alisema baada ya kuweka picha ya mama wa marehemu akilia.

Muchina alizikwa Gatundu Kusini, na Wakenya, katika wadhifa huo, walitoa wito kwa serikali kupeleka hatua kali katika kukabiliana na aina hii ya pombe.