Kijana aliyeshikwa na vazi la polisi adai alilipata katika eneo la kuuza muguka Naivasha (video)

"Nilitokelezea hapo town kwa muguka. Kijana mwenye anauza muguka, nilikuwa na home theatre yangu akaniambia nipee hiyo woofer tubadilishane na jacket." alieleza.

Muhtasari

• Hata hivyo, alikanusha kutumia koti hilo la polisi kutekeleza visa vya uhalifu akijifanya kuwa afisa wa polisi.

Kijana ashikwa na nguo za polisi.
Kijana ashikwa na nguo za polisi.
Image: Screengrab

Vijana wawili katika kaunti ndogo ya Molo kaunti ya Nakuru wametiwa mbaroni baada ya kukamatwa wakijifanya maafisa wa polisi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa video iliyonaswa na Citizen, vijana hao, mmoja alipatikana amevalia koti ya polisi na katika maelezo yake baada ya udadisi, alikiri kwamba koti hilo alilipata katika eneo la kuuzia muguka.

Alieleza kwamba koti hilo alifidiwa na jamaa anayeuza muguka ambaye alikuwa na redio yake na akamwambia kwamba haliwezi leta shida kwani si sare rasmi ya polisi.

“Hii jacket nilipata kwa shangazi yangu nilipoenda mazishi Naivasha, hapo ndio nilitokelezea hapo town kwa muguka. Kijana mwenye anauza muguka, nilikuwa na home theatre yangu akaniambia nipee hiyo woofer tubadilishane na jacket. Nikamuuliza haiwezi kuwa na shida, akaniambia ikiwa na kitambaa cha ndani haiwezi leta shida,” kijana huyo alielezea.

Hata hivyo, alikanusha kutumia koti hilo la polisi kutekeleza visa vya uhalifu akijifanya kuwa afisa wa polisi.

Tazama video hiyo hapa chini;