Mama aomba ushauri jinsi ya kumwambia bintiye wa miaka 30 kuwa kakake ni Baba yake

Mama alieleza aliolewa na mwanamume ambaye alikuwa na watoto tayari na alikuwa amefanyiwa vasektomia. Alitaka kupata mtoto wa kwake na mumewe mpya na hivyo wakamuomba mtoto wa kambo aliyekuta kwenye ndoa kuchangia kutoa mbegu.

Muhtasari

• Alieleza kwamba mume wake alikuwa na watoto wake wawili, na hakuwa na watoto wawili hao walipofunga pingu za maisha.

Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Mama mmoja ametuma ujumbe kwa jarida moja kwa sharti la kutotambuliwa jina akiomba ushauri kuhusu jinsi ya kumwambia binti yake mwenye umri wa miaka 30 kwamba kaka yake ndiye baba yake.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halikujulikana aliandika katika kipindi cha ‘Dear Therapist’ kwenye jarida la The Atlanic ili kufafanua hali hiyo.

Alieleza kwamba mume wake alikuwa na watoto wake wawili, na hakuwa na watoto wawili hao walipofunga pingu za maisha.

Wanandoa hao 'wote walitaka kupata mtoto pamoja,' lakini kwa kuwa mume wake alikuwa amefanyiwa vasektomi miaka iliyopita, ambayo haikuweza kurekebishwa tena, iliwabidi kutafuta suluhisho lingine.

Katika barua aliyotuma kwa jarida hilo, mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa aliandika hivi:

'Hatukutaka kutumia benki ya mbegu za kiume, kwa hiyo tulimwomba mtoto wa mume wangu awe mtoaji wa mbegu’

'Tulihisi huo ulikuwa uamuzi bora zaidi: Mtoto wetu angekuwa na chembe za urithi za mume wangu, na tulijua afya ya mwana wangu wa kambo, utu wake, na akili yake. Alikubali kutusaidia katika hilo.’

'Binti yetu ana miaka 30 sasa. Tunamwambiaje kwamba "baba" yake ni babu yake, "kaka" ni baba yake, "dada" yake ni shangazi yake, na "mpwa" wake ni kaka yake wa kambo?'

Inaeleweka kwamba mwanamke huyo alimalizia hivi: ‘Mimi na mume wangu tuna wasiwasi, tumechanganyikiwa, na tunahangaika kumwambia.’

'Hili pia ni gumu kwa mume wangu, kwa sababu anataka binti yetu ajue kwamba atakuwa baba yake daima na milele.'

Kwa kujibu, mwandishi wa kipenele hicho kwenye jarida, Lori Gottlieb, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia aliyehitimu, alisema kwamba kulikuwa na ukweli mbili ambazo binti ya mwanamke huyo angelazimika kukabiliana nazo.

Sio tu ufunuo kuhusu baba yake mzazi, lakini pia kwamba 'watu anaowaita wazazi wake wamemdanganya' kwa miongo mitatu.