'Achika,' Linturi ashutumiwa kwa kumhusisha mkewe wa zamani katika kesi yake

Aliongeza: "Inapaswa kuwa sio haki kwamba mambo yako ya kibinafsi yaendelee kuja wakati wowote mambo mazito yanazungumzwa

Muhtasari
  • Khaminwa alisisitiza haja ya kuzingatia masuala muhimu ya kitaifa badala ya kushawishi uhusiano wa kibinafsi au mambo mengine yasiyohusika.
Waziri wa Kilimo Mithika Linturi mnamo Aprili 8, 2024. Picha: EZEKIEL AMING'A
Waziri wa Kilimo Mithika Linturi mnamo Aprili 8, 2024. Picha: EZEKIEL AMING'A

Waziri  wa Kilimo Mithika Linturi ameshutumiwa kwa kupuuza suala la umuhimu wa kitaifa kwa kuhusisha mambo yake ya ndoa kwenye kikao maalum cha kujadili na kupigia kura ripoti ya Kamati Maalum iliyoteuliwa kuchunguza mashtaka dhidi yake.

Mbunge  wa Bumula Jack Wamboka aliambia kamati teule ya wajumbe 11 iliyosikiza kwamba kisingizio cha Linturi kuwa mke wake wa zamani Maryanne Kitany ndiye aliyechangia msukumo wa kumwondoa afisini si haki na kinapunguza uzito wa hali hiyo.

"Nimeitazama hati iliyowasilishwa na rafiki yangu mzuri Mithika Linturi na si chochote zaidi ya barua ya mapenzi kutoka kwa mpenzi aliyekasirika. Haya ni mambo mazito yenye umuhimu wa kitaifa kupunguzwa kwa mambo ya mapenzi. Ukiachwa achika!Si haki kuendelea kumvuta bibi mwema Marianne Kitany katika suala hili. Ana haki ya kukukataa ama kukubali. Mruhusu aendelee na maisha yake." Alisisitiza Wamboka.

Aliongeza: "Inapaswa kuwa sio haki kwamba mambo yako ya kibinafsi yaendelee kuja wakati wowote mambo mazito yanazungumzwa. Mwanamke mwema anapaswa kuachwa kwa amani kwa sababu ana maisha, familia na anahitaji kuendelea."

Kauli ya mbunge huyo iliungwa mkono na mwakilishi wake wa kisheria, Wakili Mwandamizi John Khaminwa, ambaye alidai kuwa jaribio la Linturi la kuhusisha mashitaka ya kumshtaki na mambo ya kibinafsi halikubaliki.

Khaminwa alisisitiza haja ya kuzingatia masuala muhimu ya kitaifa badala ya kushawishi uhusiano wa kibinafsi au mambo mengine yasiyohusika.

"Nilikuwa nikisoma majibu yaliyowasilishwa mbele ya kamati teule na utetezi mkuu unaonekana kuwa ... kwamba 'kilicho mbele ya bunge la Kenya kushughulikia masuala mazito ya kitaifa ni kwa sababu ya mke wangu wa zamani.'Mke wangu wa zamani ndiye moja kuleta shida'.

Linturi anatuhumiwa kwa sakata ya mbolea ghushi. Linturi amesema hatawaita mashahidi wa kumtetea