Kericho: Mume akamkata mkewe masikio akidai ni mkaidi na kichwa ngumu

Kulingana na ripoti ya polisi, mshukiwa alikata masikio ya mkewe kwa madai ya kutotii na kukosa kufuata maagizo.

Muhtasari

• Akizungumza na waandishi wa habari, Nthiga alisema kuwa mshukiwa alitoroka mara baada ya kutekeleza uhalifu huo.

 
• Bosi huyo wa polisi pia alionya wakazi dhidi ya tabia ya vurugu inayohusisha kuwajeruhi watu wengine.

Panga. Silaha ya muuajiiliyotumika
Panga. Silaha ya muuajiiliyotumika
Image: MAKTABA

Kisa cha kusikitisha kilishuhudiwa katika kaunti ya Kericho eneo la Sogwet-Soin baada ya mwanamume kudaiwa kumkata masikio yote mkewe na kuingia mafichoni.

Kisa hicho kilithibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo Peter Nthiga mnamo Mei 18.

Kulingana na ripoti ya polisi, mshukiwa alikata masikio ya mkewe kwa madai ya kutotii na kukosa kufuata maagizo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Nthiga alisema kuwa mshukiwa alitoroka mara baada ya kutekeleza uhalifu huo.

Bosi huyo wa polisi pia alionya wakazi dhidi ya tabia ya vurugu inayohusisha kuwajeruhi watu wengine.

Wakati huo huo, mkuu wa polisi aliwashauri wanandoa kutatua masuala yao ya ndoa kwa amani, bila vurugu, kutafuta ushauri wa kitaalamu au kuripoti kwa mamlaka za mitaa kwa usaidizi.

Aliongeza kuwa polisi wameimarisha msako wa kumsaka mtuhumiwa huyo na watamfikisha mahakamani mara atakapokamatwa.

Tukio hilo liliwashangaza wakazi wa eneo hilo, ambao walibaini kuwa jambo kama hilo halijawahi kutokea katika jamii yao.