Papa aomba radhi kwa kuripotiwa kusema lugha chafu za chuki dhidi ya watu wa jinsia moja

Taarifa iliyotolewa na Vatican imesema Papa hakukusudia kumuudhi mtu yeyote.

Muhtasari

•Katika Kongamano la Maaskofu wa Italia, papa aliripotiwa kusema wanaume wa jinsia moja wasiruhusiwe kupata mafunzo ya ukasisi.

Papa Francis
Image: BBC

Papa Francis ameomba radhi kufuatia ripoti kwamba alitumia lugha ya dharau kwa wanaume wapenzi wa jinsi moja.

Taarifa iliyotolewa na Vatican imesema Papa hakukusudia kumuudhi mtu yeyote na kuomba msamaha kwa wale ambao "waliumizwa na matumizi ya neno".

Katika Kongamano la Maaskofu wa Italia, papa aliripotiwa kusema wanaume wa jinsia moja wasiruhusiwe kupata mafunzo ya ukasisi, na kuongeza kuwa tayari kulikuwa na hali ya hewa ya frociaggine, ambayo inatafsiriwa kama lugha ya kukera sana.

Mkutano huu ulikuwa wa faragha, lakini umeripotiwa sana.