Mwanahabari nguli Rupert Murdoch mwenye umri wa miaka 93 afunga ndoa kwa mara ya tano

Mwenyekiti mstaafu wa Fox and News Corp ,Rupert Murdoch mwenye umri wa miaka 93 amefunga ndoa kwa mara ya tano baada ya kuvunja ndoa ya awali kupitia talaka

Muhtasari

•Rupert Murdoch amefunga ndoa kwa mara ya tano na mwanabiolojia mstaafu Elena Zhukoya  Jumamosi 1,Juni 2024.

•Wanandoa hao walikutana kupitia mke wa tatu wa Murdoch, Wendi Deng, kulingana na ripoti ya Daily Mail.

•Murdoch alijiuzulu mwaka jana kama mwenyekiti wa News Corp na Fox, na kuhitimisha kazi ya miongo saba.

Rupert Murdoch
Image: Hisani

Rupert Murdoch amefunga ndoa na mwanabayolojia mstaafu  Elena Zhukova huko California,hii ikiwa ni ndoa ya tano kwa Mogul mwenye umri wa miaka 93.

Kulingana na gazeti la Los Angeles times ,mwenyekiti wa Fox and News Corp Rupert Murdoch aliyestaafu alifunga ndoa na mwanabiolojia mstaafu wa molekuli Elena Zhukova mwenye umri wa miaka 67. Ndoa yao inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya Murdoch kujiuzulu mwaka jana kama mwenyekiti wa News Corp na Fox, na kuhitimisha kazi ya miongo saba.

Murdoch  alioa mke wake wa kwanza, mhudumu wa ndege Patricia Booker, mwaka wa 1956 na kupata  mtoto mmoja, Prudence, na wakatalikiana karibu miaka kumi baadaye.

Mwaka huo huo, Murdoch alifunga ndoa na mwandishi wa habari wa Scotland Anna Torv. Ndoa hiyo ilidumu zaidi ya miongo mitatu na kuzaa watoto watatu: Elisabeth, James na Lachlan.

Ndoa yake ya nne na mwigizaji na mwanamitindo Jerry Hall, ilimalizika kwa talaka mnamo 2022 baada ya miaka sita. Hall hapo awali alikuwa mshirika wa muda mrefu wa mwimbaji wa Rolling Stones Mick Jagger.

Murdoch alichumbiwa kwa muda mfupi mwaka jana na kasisi wa zamani wa polisi wa San Francisco Ann Lesley Smith, ingawa wenzi hao walikatisha uchumba wiki kadhaa baadaye.Gazeti la Vanity Fair liliripoti kutengan.

Ndoa ya hivi karibuni ya Murdoch  inakuja chini ya mwaka mmoja baada ya Fox Corp. na News Corp. kutangaza kwamba Murdoch atajiuzulu kutoka kwa jukumu lake kuu katika kampuni hizo mbili, na kwamba Lachlan atamrithi.