Nilishangaa Serikali ilipoidhinisha ugombeaji kiti wangu wa AU- Raila

Raila ambaye ni mwaniaji wa nafasi ya juu ya AUC nchini Kenya alisema ana furaha kwamba serikali imeweka pamoja timu ya maafisa wakuu kusimamia azma yake.

Muhtasari
  • Raila alisema wakati wa mkutano wa Jumatano serikali ilishiriki naye hali na viwango vya maandalizi na kujitolea kwa serikali.
KINARA WA UPINZANI RAILA ODINGA
Image: EZEKIUEL AMING'A

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amepongeza juhudi za serikali kuendeleza azma yake ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Akizungumza Jumatano baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Masuala ya Kigeni na Masuala ya Wageni Musalia Mudavadi, Raila alisema amefurahishwa.

"Nimetiwa moyo na kiwango cha maafisa wakuu serikalini ambao wametoa usaidizi wao kwa kampeni hii. Nashukuru kwa msaada huo," Raila alisema.

Raila ambaye ni mwaniaji wa nafasi ya juu ya AUC nchini Kenya alisema ana furaha kwamba serikali imeweka pamoja timu ya maafisa wakuu kusimamia azma yake.

"Nilishangaa nilipoona serikali ya Kenya ikinikubalia kugombea. Nilitarajia wangekataa," Raila alisema.

Mudavadi alisema Raila ana stakabadhi zinazofaa na zinazohitajika kuongoza AU akisema haihusu siasa za humu nchini.

Raila alisema wakati wa mkutano wa Jumatano serikali ilishiriki naye hali na viwango vya maandalizi na kujitolea kwa serikali.

"Nilihakikishia timu hiyo kwamba nitatumia tajriba yangu na mitandao kushinda mataifa mengi niwezavyo," Raila alisema.

"Kwa kujitolea kati ya serikali na timu yangu, tutaweza kunyakua kiti."

Raila alisema walikubaliana kuhusu hitaji la ufanisi, kupunguza urasimu na kuzindua timu iliyotiwa mafuta kwenda mbele.

"Tulikubaliana juu ya hitaji la kuelewa unyeti katika azma hii iwe ya kitaifa ya kikanda, bara na kimataifa katika azma hii," alisema.

Raila alisema anawania nafasi hiyo barani Afrika na wala si katika Jamhuri ya Kenya."....lakini ninahitaji kuidhinishwa na serikali ya Kenya kwa nafasi hiyo," alisema. Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi alisema Raila ana stakabadhi zinazofaa na zinazohitajika kuongoza AU akisema haihusu siasa za humu nchini.

"Tulisema ndiyo kwa sababu Raila amefuzu na ni Mkenya. Hii haihusu siasa za humu nchini, inahusu maslahi ya kitaifa,'' alisema.