Siaya: Mwanamume aingia katika kanisa la Kikatoliki na kunya kwenye sanamu ya Yesu!

Polisi walisema picha za CCTV zilimuonyesha mwanamume huyo wa umri wa makamo aliichukua sanamu hiyo kisha kujisaidia haja kubwa juu yake na kuificha chini ya viti kanisani kabla ya kuondoka.

Muhtasari

• “Kisha alijisaidia haja kubwa kwenye sanamu kabla ya kuondoka kanisani. Aliificha sanamu iliyoharibiwa chini ya viti,” polisi walisema.

• Mshukiwa huyo anasemekana alikwenda kwenye jumba la juu la sanaa ambapo alikuwa ameificha sanamu hiyo.

• Kisha akaonekana akishuka kwenye madhabahu ambako aliichukua sanamu.

Sanamu ya Yesu ukutani
Sanamu ya Yesu ukutani
Image: BBC

Taharuki na mshangao vilitanda katika kanisa moja kwenye kaunti ya Siaya baada ya mwanamume mwenye umri wa makamo kuripotiwa kuingia kanisani na kunya kinyesi kwenye sanamu ya Yesu Kristo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, tukio hilo la kushangaza lilijiri katika kanisa moja la kikatoliki kwenye kaunti ndogo ya Bondo.

"Kitendo hicho cha kikatili kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Bondo na kasisi wa parokia hiyo," Citizen walimnukuu kamanda wa polisi katika kaunti ya Siaya.

Kamanda wa polisi aliongeza kuwa ripoti zaidi zinaonyesha kuwa sanamu hiyo ambayo imekuwa kwenye madhabahu ya kanisa hilo iliripotiwa kutoweka.

"Baada ya kukagua picha za CCTV, ilibainika kuwa mgeni ambaye alikuwa amevalia shati la mistari nyeusi na nyeupe na suruali nyeusi aliingia katika ukumbi wa kanisa wakati waumini wachache walikuwa wakisali sana," aliongeza.

Mshukiwa huyo anasemekana alikwenda kwenye jumba la juu la sanaa ambapo alikuwa ameificha sanamu hiyo.

Kisha akaonekana akishuka kwenye madhabahu ambako aliichukua sanamu.

“Kisha alijisaidia haja kubwa kwenye sanamu kabla ya kuondoka kanisani. Aliificha sanamu iliyoharibiwa chini ya viti,” polisi walisema.

Juhudi za kumtafuta mshukiwa zilikuwa zinaendelea mpaka wakati taarifa hii inachapishwa.