Bwana Harusi afunga harusi bila bibi harusi baada ya kukosana dakika za mwisho

Taarifa ilisema kwamba bwana harusi alikuwa amelipa mahari ya takribani milioni moja na salio la laki mbili ndilo lilibaki na kuzua mvutano baina ya pande mbili husika.

Muhtasari

• Lakini cha kushangaza, bwana harusi alishikilia msimamo wake kwamba harusi lazima ingeendelea kama ilivyopangwa licha ya kutkowepo kwa bibi harusi.

BWANA HARUSI
BWANA HARUSI
Image: AYO TV

Harusi isiyo ya kawaida ilishuhudiwa katika mkoa wa Katavi nchini Tanzania ambapo bwana harusi aliamua kufunga harusi licha ya kutokuwepo kwa bibi harusi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyopeperushwa kwenye Ayo TV, Edward Futakamba, mkaazi wa manispaa ya Mpanda aliwashangaza wengi baada ya kuamua kuendelea na mipango ya kufanyika kwa harusi yake licha ya bibi harusi kugoma kuhusika.

Jamaa huyo aliarifiwa kwamab alikuwa akiishi na mwanamke huyo na kupata mtoto wa kike ambaye sasa ana umri wa miaka 3 ambapo baadae waliamua kufunga ndoa na taratibu zote kuanza kfuuatwa ikiwemo kutoa mahari na tarehe ya harusi kutangazwa kuwa Julai 26.

Hata hivyo, siku nne kabla ya siku ya harusi, upande wa bibi harusi ulituma taarifa kwa kamati ya maandalizi ya harusi hiyo wakisema kwamba hawakuwa na nia ya kuhusika kaitka harusi hiyo hivyo kupeleka pingamizi kanisani.

Lakini cha kushangaza, bwana harusi alishikilia msimamo wake kwamba harusi lazima ingeendelea kama ilivyopangwa licha ya kutkowepo kwa bibi harusi.

“Tulijaribu kuwatafuta na kuzungumza naoi li angalau hili jambo liende kama lilivyokuwa lakini ikashindikana, sasa tukaona kwamba haiwezekani kwamba watu wametoa michango yao halafu hawa wakatishe hili suala. Hatujajua shida kwao ni nini lakini kwa upande wetu tulikuwa mahari tumelipa na kila kitu, nafikiri ilikuwa imebaki kama laki mbili katika hiyo mahari,” mmoja wa wanakamati andalizi alisema.

Kwa upande wake, bwana harusi alisema kwamba ilibidi tu asherehekee kama alivyoratibu kwani yote ni makusudio ya Mungu.

“Kupata na kukosa yote ni sehemu ya maisha, na cha msingi sana ikiwa kama mtu unaweza kufurahia na kusherehekea ukiwa umepata, basi ni vizuri pia haka ukiwa umekosa usherehekee na kufurahia pia kwa sababu mpango wa Mungu yeye ndiye anayejua. Ndicho kitu mimi nilichokifanya, hivi nimemshukuru Mungu kwa kila jambo,” bwana Futakamba alisema.

Hii hapa video ya tukio hio;