Video ya mbunge Salasya akimpiga kofi moto mwombolezaji yazua ghadhabu (+video)

"Wewe enda kaa chini sasa.Nani enda kaa chini. Enda kaa chini sasa!!,” Salasya alimwagiza mwombolezaji huyo kabla ya kumpiga kofi.

Muhtasari

•Salasya alionekana akimpiga kofi mwanasiasa wa eneo hilo la kaunti ya Kakamega ambaye pia alijitokeza katika hafla hiyo.

•Mwombolezaji huyo alijaribu kumkabili Salasya lakini alizuiwa na walinzi wenye miraba minne waliokuwa wameandamana na mbunge huyo.

alimpiga kofi mwombolezaji siku ya Ijumaa.
Mbunge Peter Salasya alimpiga kofi mwombolezaji siku ya Ijumaa.
Image: HISANI

Kanda ya video inayomuonyesha Mbunge wa eneo la Mumias East Peter Salasya akimchapa kofi mwombolezaji mmoja katika hafla ya matanga ambayo alihudhuria siku ya Ijumaa imezua hisia mseto kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Radio Jambo imeweza kubaini kuwa mwanamume aliyepokea kofi hilo moto kutoka kwa mbunge huyo kijana ni mwanasiasa wa eneo hilo la kaunti ya Kakamega ambaye pia alijitokeza katika hafla hiyo.

Hali ya kutoelewana iliyopelekea vita vya kimwili ilitokea baada ya kiongozi huyo wa eneo hilo kudaiwa kutaka kuzungumza pia wakati Salasya alikuwa akitokea hotuba yake.

“Kwanza nataka nichukue hii nafasi niambie familia pole sana. Mimi nimekuwa hapa, nakumbuka wakati nilikuwa pale mama alikuwa wa heshima sana na alinikaribisha hapa nyumbani na nilikuwa na furaha sana. Na kwa sababu ya hiyo, mimi nimesema, hata kama leo nimekuwa na kazi nyingi, mpaka leo nifike hapa niomboleze na familia. Sasa nataka nimuombe Mungu Roho ya mtumishi ipumzike pema,” Salasya alisikika akiwaambia waombolezaji kabla ya kuanza kumuamuru mwanasiasa huyo wa eneo hilo aliyesimama mbele yake aketi.

Salasya alisikika akimuamuru mwanaume huyo, “Wewe enda kaa chini sasa. Enda kaa chini. Nani enda kaa chini. Enda kaa chini sasa!!,” kabla ya kumpiga kofi moto sana kwa kutumia mkono wake wa kulia.

Baada ya kupokea kofi hilo, mwanasiasa huyo alijaribu kumkabili Salasya lakini alizuiwa na walinzi wenye miraba minne waliokuwa wameandamana na mbunge huyo.

Kelele na mayowe vilitanda huku waombolezaji wakishuhudia mzozo huo.

Video za tukio hilo sasa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hisia tofauti kutoka kwa watumiaji wa mtandao huku wengi wakionekana kukosoa kitendo cha mbunge huyo.

Tazama maoni ya baadhi ya watumizi wa mtandao wa X;

@KBonimtetezi: Our leaders have gone mad. From an MP shooting a DJ to another one shooting a man dead, to others pitting rival goons against each & now to this! Kenyan voters must seriously retrospect.

@RodgersKipembe: Salasya power imemuingia kichwa hadi sasa analima constituents makofi kwa matanga. Sad.

@KinyanBoy: Salasya is everything okay at home? This now how a leader behaves, you’re an MP not a street urchin.

@Josh001J: MP Salasya alikulisha constituent wake kofi jana hadi ikatoa echo manze😭

@KILUNDEEZY: Leaders are now becoming ungovernable lakini hiyo kofi bana,who has a better view