Acheni kuwahangaisha wafuasi wangu-Ruto awaambia polisi

Muhtasari
  •  Ruto ataendelea na msururu wa kampeini zake maeneo ya Kisii na Magharibi 
  • Amesema hatotishwa na 'maafisa wenye uchu wa maamlaka'
  • Ruto amewataka polisi kukoma kutumiwa vibaya na 'mabroka wa kisiasa'

 

Naibu wa Rais William Ruto na wabunge Didmus Baraza na Dan Wanyama

 

Naibu wa rais William Ruto  amewataka polisi kukoma kuwahangaisha wafuasi wake na kungilia kazi yake . Akizungumza siku ya jumanne katika makaazi yake ya Karen  alipokutana na viongozi kutoka kaunti ya Narok ,Ruto  amesema kuna njama ya kuendeleza ghasia za kisiasa na kumtwika lawama .

  Viongozi wanaoiunga mkono serikali wanamtaka Ruto kuwajibikia rabasha ziliztokea huko Kenol katika kaunti ya Murang’a siku ya jumapiliu ambako watu wawili waliuawa baada ya makundi ya vijana kushambuliana .

 
 

 Ruto alitoa mfano wa ghasia za mwezi  jana huko Kisii muda mfupi kabla ya kuwasili kwake kama ushahidi kwamba polisi wanaingilia hafla zake na kusababisha machafuko .

Ruto,  anatarajiwa kufanya tena ziara nyingine za kampeini katika sehemu mbali mbali za nchi  na amemtaka mkuu wa polisi Hillary Mutyambai  kukoma kuchukua maagizo kutoka kwa  ‘mabroka wa kisiasa  na maafisa wa serikali wenye uchu wa maamlaka’ .

 Amesema idara za usalama zinawajua waliotekeleza ghasia huko Kenol na wanafaa kuchukuliwa hatua . Amehutia kwamba polisi wanatumiwa kutekeleza  ‘oparesheni za kisiasa’ huku akimtaka Mutyambai kusimamia haki na kuwhaudumia wakenya wote bila ubaguzi .

 Kuanzia alhamisi Ruto  ataanza msururu wa ziara huku akitarajiwa kwenda Nyamira anakotoka waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I  na siku ya ijumaa atarejea Kisii ambako alikuwa amefanya ziara nyingine mwezi uliopita .

 Siku ya jumapili Ruto atakuwa kakamega kwa hafla ya  kuchangisha fedha za kanisa la  St Joseph Catholic eneo la  Dangalasia Koyonzo kaunti ndogo ya Matungu .

 Kutoka matungu Ruto ataelekea  Mumias mashariki ambapo mbunge wa eneo hilo  Benjamin Washiali