- Rais Uhuru ameipokea Ripoti ya BBI leo
- Amesema wakenya wanafaa kuisoma wenyewe
Rais Uhuru Kenyatta amewakosoa wanaopinga ripti ya BBI akisema wanafaa kuonyesha uongozi wanaposisoma ripoti hiyo badala ya kusababisha migawanyiko .
Uhuru amesema hatozungumza kuhusu yaliyomo katika ripoti hiyo ili watu wasimshtumu kwa kushawishi matokeo yake
" Hatuangalii mambo ambayo yanatugawanya . Tulete mwafaka ili tusonge mbele .Nataka kuwaraia wanasiasa wenzangu kwamba huu sio wakati wa kuleta migawanyiko’
Rais aliyasema hayo siku ya jumatano akipokea ripoti ya BBI na kiongozi wa upinzani Raila Odinga huko Kisii .
" Huu ni wakati wa kuwaleta wakenya pamoja .Naipokea hii ripoti kwa mara ya kwanza . ndio kwa sababu tulinyamaza kuihusu kwa ajili ya imani yetu kwenu..
Tusiiache nafasi hii kuhariika kwa sababu ndogo ndogo za kisiasa’
Uhuru amesema wakenya wanafaa kuisoma ripoti hiyo kwa makini na kisha kujifanyia maamuzi .
Rais amesema wakenya wanafaa kuisoma ripoti ya BBI kivyao na sio kuegemea misimamo yao ya kisiasa na kutoa maoni yao ili kuiboresha
" Leo tunaipokea ripoti hii lakini siku ya jumatatu tutapata fursa huko Bomas ili kusomewa yaliyomo hatua kwa hatua’ Uhuru amesema