Covid 19

18 waaga dunia kwa ajili ya corona huku 276 wakipatikana na virusi hivyo

sampuli 2,126 zimepimwa

Muhtasari

 

  •  Leo watu 220 wamepona ugonjwa  huo
  • Kwa sasa kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha ICU  ,52  wanaosaidiwa kupumua
  •  Jumla ya watu 1,191 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini ilhali  1,406 wapo chini ya utunzi wa nyumbani

 

Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe Mutahi Kagwe

Watu 276 wamepatikana na virusi  vya corona siku ya jumatatu baada ya sampuli 2,126 kupimwa katika saa 24 zilizopita  na kufikisha visa hivyo nchini kuwa 49,997 na jumla ya idadi ya sampuli zilizopimwa kuwa 662,046 .

Kutoka visa hivyo 273 ni vya wakenya ilhali 3 ni vya raia wa kigeni . watu 179 ni wanaume ilhali 97 ni wanawake .mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 90 .

 Leo watu 220 wamepona ugonjwa  huo na kufikisha 34,429 jumla ya idadi ya waliopona .

 Hata hivyo watu 18 wamega dunia na kufikisha 920 idadi ya walioangamizwa na corona hadi kufikia sasa

 Kwa sasa kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha ICU  ,52  wanaosaidiwa kupumua na  20 katika kitengo cha HDU . Jumla ya watu 1,191 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini ilhali  1,406 wapo chini ya utunzi wa nyumbani