Uchungu wa mama

‘Msituache na Uchungu’ asema mamake Baby Pendo wakati wa uzinduzi wa BBI

wazazi wake Pendo walikuwa miongoni mwa waliozungumza Bomas

Muhtasari
  • Joseph Abanta amesema wakenya ni watu wazuri na hawafai kukubali kuhadaiwa au kutumiwa vibaya na viongozi wa kisiasa
  • .Mkewe alilazimika  kutoka nje kwa moshi mkali uliokuwa umetanda katika nyumba yao

 

Mamake Baby Pendo Lencer Achieng wakati wa uzinduzi wa ripoti ya BBI katika ukumbi wa Bomas

 

Mamake Pendo Lancer Achieng amesema hakuna kitakachoweza kumrejesha mtoto wake .  Achieng amesema hakuna mwanamke anayefaa kuomboleza kifo cha mtoto wake , amezungumza wakati wa uzindzi wa ripoti ya BBI katika ukumbi wa Bomas

 Babake mtoto Pendo ambaye aliuawa kwa kupigwa rungu na polisi wakati wa machafuko ya uchaguzi mkuu uliopita amewashauri wakenya kutohadaiwa na wanasiasa .

Joseph Abanta amesema wakenya ni watu wazuri na hawafai kukubali kuhadaiwa au kutumiwa vibaya na viongozi wa kisiasa .

‘ Acheni damu ya mtoto wangu iwe  wakati wa mwisho mtu kupoteza maisha yake kwa sababu ya siasa’ amesema Abanta

Abanta amemrai rais Uhuru kutozisahau familia za  waaithiriwa wa ghasia za uchaguzi wakati huu mgumu

"Naomba Rais Uhuru vile mumeshikana na Raila Odinga msiachane mkono. Naona BBI italeta mabadiliko kwa maisha yetu. Rais kumbuka familia ya Baby Pendo msituache hivo. Mumetuacha tunateseka,”  amesema

Baby Pendo,  aliuawa wakati polisi waliokuwa wakshika doria walipovamia nyumba  yao . walikuwa wamelala mwendo wa saa sita unusu usiku waliposikia ukemi wa  jirani yao aliyekuwa amevamiwa  na wakaamka .

 Wazazi wake  Lencer Achieng na Joseph Abanja  walijaribu kuzuia polisi wasiingie katika nyumba yao kwa kuweka kitanda karibu na mlango lakini walizidiwa nguvu .

 Polisi baadaye walitupa kitoa machozi ndani ya nyumba yao  na kufunga mlango kutoka nje .Familia hiyo ya watu wanne ilijaribu kujinasua   lakini  Abanja alipofaulu kutoka nje alijipata mikononi mwa polisi waliokuwa wamemngoja kwa rungu  .Mkewe alilazimika  kutoka nje kwa moshi mkali uliokuwa umetanda katika nyumba yao