Faini

Valia maski au upigwe faini ya shilingi 20,000-Mutyambai

Mutyambai amesema polisi hawafai kutumia nguvu kupindukia

Muhtasari

 

  •  Visa zaidi vya corona vinaripotiwa kila siku 
  • wakenya wengi waepuuza kanuni za kupambana na corona 

 

 

Mutyambai
IG Hillary Mutyambai Mutyambai

 

Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai amewaonya  wananchi dhidi ya kutovalia maski   katika maeneo ya umma  . IG amesema  kupitia twitter  kwamba wanaokosa kuvalia maski katika sehemu za umma watapigwa faini ya shilingi 20,000 

 Hata hivyo  amesema polisi wanafaa kutekeleza kanuni hiyo ila wasitumie nguvu kupita kiasi .

Mutyambai  pia amewataka wananchi kuripoti visa ambavyo polisi wanatumia nguvu kupindukia wakitekeleza agizo hilo  kwa afisi yake  IAU, au IPOA  kwa hatua kuchukuliwa

 Onyo hiyo yake inajiri huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kulihutubia nchi kuhusu ongezeko la visa vya corona .

 Rais ameitisha mkutano na magavana ili kujadili visa vipya vya corona nchini  .msemaji wa Ikulu Kanze Dena wiki jana alisema mkutano huo utafanyika tarehe nne  mwezi huu .

 Taifa kwa sasa imesajili visa Zaidi vya corona na vifo Zaidi ya 1000