Korokoroni

Mgombeaji wa Urais Uganda Bobi Wine akamatwa

Wine alikuwa ameshawasilisha stakabadhi zake kwa tume ya uchaguzi

Muhtasari

 

  •  Msemaji wa polisi Luke  Owoyesigire  amesema hawajapokea maelezo kuhusu kukamatwa kwa Wine na kuahidi kutoa taarifa baadaye .
  • Wine,  mwenye umri wa miaka 38,  ni mwanamuziki  ambaye jina lake halisi  Robert Kyagulanyi,  analenga  kumaliza uongozi wa rais Yoweri Museveni
  • Museveni pia alipewa idhini kutetea kiti chake siku ya jumatatu

 

 

Bobi Wine

 

Mgombeaji wa urais wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amekamatwa na polisi  baada ya kukabidhi stakabadhi za ugombeaji kwa tume ya uchaguzi nchini humo ,msemaji wa chama chake amesema

" Walitumia nyundo kuvunja dirisha la gari lake  na kumvuta …na kumweka katika gari lao na kuondoka ‘ Amesema  Joel  Senyonyi msemaji wa chama cha NUP .

 Msemaji wa polisi Luke  Owoyesigire  amesema hawajapokea maelezo kuhusu kukamatwa kwa Wine na kuahidi kutoa taarifa baadaye .

Wine,  mwenye umri wa miaka 38,  ni mwanamuziki  ambaye jina lake halisi  Robert Kyagulanyi,  analenga  kumaliza uongozi wa rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 34 . Uchaguzi nchini humo utafanyika  Februari mwaka ujao .

 Wine amefaulu kuwavutia  wafuasi wengi kwa sababu ya umaarufu wake katika muziki  ,hatua ambayo imekishtua chama tawala cha NRM  ambacho kupitia vyombo vya usalama kimeanza msako dhidi ya wafuasi na viongozi wa upinzani . Tangu msanii huyo alipotangaza niayake kugombea urais ,polisi na jeshi wamekuwa wakifanya oparesheni za kuwatawanya wafuasi wa upinzani katika mikutano ya hadhara .Museveni pia alipewa idhini kutetea kiti chake siku ya jumatatu