Kassait aidhinishwa na bunge

Wabunge waidhinisha uteuzi wa MPs Kassait kama kamishna wa Data

mabalozi wengine 14 pia wameidhinishwa na bunge

Muhtasari

 

  • Kamati ya ulinzi  inayoongozwa na mbunge wa kajiado kusini Katoo Ole Metito iliidhinisha  uteuzi wa  mabalozi 14 walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta .
  • Wengine ni balozi  Tom Amollo (Berlin), Tabu Irina (Tokyo), na Lindsay Kiptiness (Bangkok).

 

Immaculate Kassait

 

 Kamati  moja ya bunge imeidhinisha  uteuzi wa Immaculate Kassait kama kamishna wa Data  na wengine 14 walioteuliwa  kuhuduu kama mabalozi .

 Kamati ya bunge kuhusu mawasiliano  imeidhinisha uteuzi wa Kassait  ambaye hadi uteuzi wake alikuwa mkurugenzi  wa usajili wa wapiga kura katika tume ya uchaguzi na mipaka .

 

 Kamati ya ulinzi  inayoongozwa na mbunge wa kajiado kusini Katoo Ole Metito iliidhinisha  uteuzi wa  mabalozi 14 walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta .

  Kamati hiyo  pia iliidhinisha uteuzi wa  wa  Maj Gen. (Rtd) Samwel Nandwa (Juba), Stella Munyi (Harare) and Daniel Wambura (Bujumbura), John Tipis (Cabberra), Benson Ogutu (Moscow), Immaculate Wambua (Ottawa), Catherine Mwangi (Pretoria, South Africa) na  Martin Kimani (United Nations New york).

 Wengine ni balozi  Tom Amollo (Berlin), Tabu Irina (Tokyo), na Lindsay Kiptiness (Bangkok).