Mihadarati

Mwanamume akamatwa na kilo tatu za Heroin JKIA

Mshukiwa yuko seli

Muhtasari
  •  Alikamatwa na maafisa wa kitengo cha kupambana na mihadarati JKIA 
  •  DCI imekuwa ikiwakamata washukiwa wengi wa ulanguzi wa dawa za kulevya katika uwanja huo 

 

Polisi wamemkamata mwanamme mmoja aliyekuwa na kilo tatu za dawa ya kulevya ya ‘unga’ inayoshukiwa kuwa heroin .

Ordijhe Mike  ambaye alikuwa akisafiri kuelekea nchini Italia alikamatwa katika uwanja wa JKIA    maafisa wa DCI wamesema kupitia Twitter .

 Alikamatwa na maafisa wa kitengo hicho kutoka kikosi cha kukabiliana na dawa za kulevya chenye makao yake uwanjani humo . DCI   imezidisha vita vyake dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya kwani imefanya msururu wa unasaji wa washukiwa wa ulanguzi wanaotumia uwanja huo kuingiza ama kutoa nje ya nchi dawa za kulevya .

 Mwezi jana heroin iliyokuwa imefichwa katika nguo za washukiwa ilinaswa katika uwanja Huo ikipelekwa katika nchi za Sudan Kusini na Ufaransa.